Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Baskeli
Kijana Mlemavu Badri Ameir Issa ambayo itamsaidia katika harakati zake
za Kimaisha. Msaada huo amekabidhiwa katika Nyumba ya kurekebishia Tabia
iliyopo Nyarugusu Shehia ya Pangawe Wilaya ya Magharibi. Kushoto ni Mlezi Mkuu wa Nyumba hizo Bibi Fatma Sukwa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
Viongozi pamoja na Vijana wanaoishi katika Nyumba za kurekebisha Tabia
kwa watu waliokuwa wakitumia dawa za kulevya { Sober House } zilizopo
Nyarugusu Wilaya ya Magharibi.
Balozi
Seif Ali Iddi akimkabidhi vyakula Mshauri Mkuu wa Nyumba saba za
kurekebishia Tabia Unguja na Pemba Bibi Fatma Sukwa kwa ajili ya
kusaidia Vijana wa nyumba hizo. Wa kwanza kushoto ni mlezi wa Nyumba ya
kurekebishia watu waliotumia dawa za kulevya ya Mtaa wa Nyarugusu
Shehia ya Pangawe Bw. Badru Nassor Ali.
**************************
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuwasaidia Vijana waliotengemaa
baada ya kuacha matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwapatia mtaji endapo
vijana hao wataamaua kubuni na hatimae kuanzisha miradi ya kujiimarisha
Kiuchumi.
Kauli
hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi wakati akizungumza na Viongozi na baadhi ya Vijana waliomo katika
nyumba saba za kurekebishia tabia Unguja kwa watu
waliokuwa wakitumia dawa za kulevya, katika moja ya nyumba hizo
iliyopo Mtaa wa Nyarugusu Shehia ya Pangawe Wilaya ya Magharibi.endelea kupitia audiface jackson blogspot kwa habari zaidi..Balozi
Seif amesema Serikali kupitia Wizara inayosimamia masuala ya Ajira ina
mpango wa kuwawezesha Wananchi hasa Vijana kujiendesha kimaisha katika
dhana nzima ya kuwajengea mazingira ya kuchapa kazi kwa vile Vijana ndio
nguvu kazi kubwa inayotegemewa na Taifa.
Amesema
kazi kubwa inaendelea kufanywa kupitia Taasisi, Jumuiya Washirika wa
Maendeleo kwa kushirikiana na Serikali ya kubadilisha tabia kwa Watu na
hasa Vijana kuacha kuendelea kutumia dawa za kulevya.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameshauri kuwa ipo haja kwa Jamii kwa
kushirikiana na Serikali Kuu pamoja na washirika wa Maendeleo kutafuta
mbinu za kuwajengea mazingira bora Vijana walioacha matumizi ya dawa
hizo ili wajiepushe kurejea katika magenge ya kihuni.
Mapema
Mlezi Mkuu wa Nyumba saba za kurekebishia Watu wanaotumia dawa za
kulevya Zanzibar Bibi Fatma Sukwa alisema asilimia 42% ya watu
waliopitia katika Nyumba hizo wameacha matumizi ya Dawa za kulevya
katika kipindi cha miaka mitatu.
Bibi
Fatma alifafanua kwamba asilimia 48% ya Vijana waliopitia Nyumba hizo
wamerejea kutumia dawa za kulevya baada ya kutengwa na Familia zao,
asilimia 1% hadi sasa hawajuilikani taarifa zao tokea waondoke katika
Nyumba hizo.
Mshauri
huyo Mkuu wa Nyumba za kurekebishia tabia kwa watu waliotumia dawa za
kulevya ameitahadharisha Jamii kuelewa kwamba dawa za kulevya ni ugonjwa
kama magonjwa mengine yanayo wazunguka wanadamu.
Kwa
upande wake Mshauri wa kuacha dawa za kulevya na kubadilisha tabia
katika nyumba saba za kurekebishia tabia za Unguja na Pemba Bw. Ahmed
Islam ameema Jamii inapaswa kuacha tabia ya kuwanyooshea vidole Vijana
walioathirika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Bw.
Ahmed Islamu amempongeza na kumshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif kwa msaada wake ambao ni faraja kwao ukionyesha
kuyathamini makundi hayo ya Vijana.
Post a Comment