Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JAJI MFAWIDHI WA KANDA YA ARUSHA ATAKA WANACHI WATOE MAONI YA KATIBA MPYA


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aisha Nyerere(katikati)
akipokea maandamano wakati wa maadhimisho ya miaka 17 ya kituo cha Kisheria cha Haki za Binadamu(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hichoDk.Hellen Kijobisimba na (kulia) ni KAimu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi LHRC Wakili Francis Stolla ambaye pia ni Rais wa Chama cha MawakiliTanganyika(TLS)
PICHA NA ASHURA MOHAMED-ARUSHA
……………………………………………
Na Ashura Mohamed,Arusha
JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Jaji Aisha Nyerere,amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuweza kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni juu ya katiba mpya.
 Aidha mashirika,taasisi zilizo za kiserikali au zisizokuwa za kiserikali kutumia nafasi zao kuisaidia serikali kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mchakato huo.
 Jaji Nyerere ameyasema hayo juzi mjini hapa wakati alipokuwa akizindua vitabu vya uwajibikaji wa makampuni kwa jamii pamoja na kitabu kinachohusu haki za jamii katika maeneo ya uwekezaji,uzinduzi ulioenda sambamba na maadhimisho ya miak 17 ya Kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC).
  Jaji huyo amesema kuwa watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali hivyo wanapaswa kuungwa mkoni kwani utetezi wa haki za binadamu ni wajibu wa jamii nzima.

 Aidha amefafanua kuwa watetezi wa haki za binadamu wanaweza kuisaidia serikali katika uendelezaji na kulinda haki za binadamu na ni nafasi pekee kutengeneza misingi imara ya kuwatetea na kuwalinda watetezi wa haki za binadamau na kuna nafasi nzuri kama wakati huu wa mchakato wa kuhakikisha kuwa haki za binadamu na matamko mbalimbali ya kimataifa yanaridhiwa na kuwekwa katika katiba mpya kwani hii itakuwa na mchango mkubwa sana katika kulinda haki za binadamu na watetetzi wa haki hizo.
 Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Dk.Hellen Kijobisimbo amesema kuwa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili katika kutekeleza majukumu yao ni pamoja na sheria kuwa kandamizi,hata wanapokuwa wanamsaidia mtu kisheria,sheria zimekuwa zikiwakandamiza.
 Pia wametaja changamoto nyingine kuwa ni tatizo la mfumo wa mahakama ambapo mashauri yamekuwa yakichukua muda mrefu hadi kukamilika,wasaidizi wa kisheria kutokutambulika.
 Dk.Hellen ameongeza kuwa vyombo vya dola navyo vimekuwa ni tatizo kwao kwani wakati mwingine wao wakiwa katika majukumu yao ya utetezi,vyombo vya dola vimekuwa vikiwaona wao ni wapinzani wakati wao ni wasaidizi wa serikali.
 Naye Mratibu wa Kitengo cha uwajibikaji wa makampuni na mazingira(LHRC) Wakili Flaviana Charles akizungumza wakati wa uzinduzi wa vitabu hivyo amesema kuwa  sheria ya uwekezaji hapa nchini haina vifungu vyenye kutoa wajibu wa wawekezaji kwa wananchi jambo linalosababisha jamii kutokunufaika na miradi ya uwekezaji inavyotekelezwa katika maeneo husika.
 Ameongeza kuwa ukosefu wa sheria inayosimamia uwajibikaji wa makampuni kwa jamii umepekelea kuwepo kw ugumu wa kuzichukulia hatua za kisheria kampuni zinazoshindwa kutimiza wajibu wake kwa jamii,ambayo imesababisha uwepo kwa migogoro isiyoisha ndani ya jamii.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top