 |
Mwili
wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima, Agness
Christopher Yamo umeagwa leo mchana Buguruni, Dar es Salaam, tayari kwa
safari ya mazishi kesho mjini Morogoro. Yamo aliyewahi pia kufanya New
Habari 2006 Limited, alifariki dunia jana katika hospitali ya Jeshi,
Lugalo, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Katika
uagwaji wa mwili wa marehemu, aliyekuwa mcheshi na rafiki wa wengi,
mamia walijitokeza na wengi walishindwa kujizuia kiasi cha kulia hadi
kupoteza fahamu. Hakika ilikuwa huzuni, simanzi na majonzi eneo la
tukio. Agness ameliza watu. Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu,
Amin. PICHA KWA HISANI YA BIN ZUBERY BLOG |
on Wednesday, September 26, 2012
Post a Comment