……………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), amekabidhi mabati kwa kikundi cha gongagonga cha Mwanzange pamoja na vifaa vya michezo kama njia ya kuwawezesha wajasiriamali hao.
Akizungumza leo jiji hapa baada ya
kukabidhi mabati hayo kwa diwani wa kata ya Mwanzange Rashid Jumbe
(CUF), mbunge huyo alisema kuwa taifa haliwezi kuendelea bila kuandaa
utaratibu mzuri wa kuwathamini wajasiriamali wadogo wadogo wa nchini.
Alisema mabati hayo kwa kikundio
hicho ni sehemu ya ahadi yake kwa wajasiriliamali hao ambao walitaka
wapatiwe bati kumi ili waweze kujenga banda ambalo litawasaidia
kuwakinga na jua pamoja na mvua.
“Ninajisikia furaha kutoka ndani
ya nafsi nyangu leo hii kuweza kuwakabidhi mabati haya yenye thamani ya
Sh 170,000 kwa na ninajua huu ni mwanzo najua tutakutana tena ili kuweza
kutekeleza na mengine zaidi.
“Kama mnavyofahamu kuwa taifa
lolote ili liweze kuendelea ni lazima liandae mazingira mazuri kwa
wajasiliamali wake hasa vijana nja wanawake ambao ndiyo nguvu kazi ya
Taifa na kama nilivyokuja na kuaniambia niwaletee nini sasa nimeanza na
utekelezaji wa ahadi yangu hii kwenu.
“Mbali an hatua hii sasa
ninachowaomba anzeni harakati za kusajili Saccos, ili kuweze kukopesheka
na taasisi za fedha name kama Mbunge wenu nitawasaidia kwa kulisimamia
hili kwa nguvu zangu zote,” alisema Mwidau.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya
Mwanzage Rashid Jumbe (CUF), alimshuruku mbunge huyo kutekeleza ahadi
yake kwa wakati huku akiamuahidi atahakikisha nasimamia utekelezaji wa
uanzishwaji wa Saccos kwa wajasiriamali wa gongagonga.
“Ninajua wapo wengi lakini mbunge
wetu Mwidau, umeonyesha mfano wa kuigwa kwani umeweza kutekeleza hili
katika kipindi kifupi tangu ulipokuja hapa na kuzungumza na
wajasiriamali hawa,” alisema Jumbe.
Post a Comment