……………………………………………..
ALIYEKUWA muasisi wa Chama cha Mageuzi ya Kitaifa (NCCR-Mageuzi), Emmanuel Petro Ole Sirikwa amefariki dunia juzi kwenye hospitali ya AICC jijini Arusha alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi.
Akizungumza na wandishi wa habari kwenye ofisi za Chama hicho jijini Dar es Salaam jana Naibu Katibu Mkuu kwa upande wa Zanzibar, Mussa Kombo Mussa, alisema chama kimepoteza mwanamageuzi wa kweli katika ulingo wa siasa nchini.
“Chama kimempoteza mtu muhimu, alikuwa ndiye kinara alikuwa miongoni mwa wanchama mwenye kadi Na. 3 za mwanzo kwani waliokuwa na kadi Na.1 na Na. 2, ni wale waliyojiingiza kwenye misuko suko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi iliwafanya wamsaliti mtoto waliyemzaa (NCCR-Mageuzi) na kukimbilia vyama vingine”alisema Mussa.
Mussa alisema Ole Sirikwa alifariki usiku wa kuamkia Oktoba 28 mwaka huu katika hospitali hiyo, ambako alilazwa kwa majuma mawili baada ya kuugua ugonjwa huo kwa muda mfupi.


Post a Comment