ACHENI NIWAPE HESHIMA WANAWAKE WOTE DUNIANI KWA YANAYOWAKUTA:
Imagine:
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza, anakuelewa,anakusamehe - halafu anasahau.
UNAZAA NJE YA NDOA:
Anasononeka na kulia sana. Anachukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu
analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa mtoto, si wewe
uliyefanya umalaya!
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI:
Anakukaribisha,anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER:
Anakuandalia staftahi (saa nyingine
unagoma kutumia staftahi yake) Unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na
kuzimua. Wala halalamiki!
CHAKULA CHA USIKU:
Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho
yake tena inaweza kutokea. Hana kinyongo!
UNAJIANDAAA KWENDA KIBARUANI:
Unakuta kashakuandalia viwalo, suruali imenyooshwa kama
ya askari
trafik, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa
tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
UNAMPA UJAUZITO:
Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuchia wewe
umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na
pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na
mwingine tena! Na mengine meeeenggggiiiiii sana wanafanyiwa hawa watu
lakini
WANASAMEHE, WANAVUMILIA!
Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwangu!
HIVI INGEKUWA WANAUME WANAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?
Anakukaribisha,anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake) Unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!
yake tena inaweza kutokea. Hana kinyongo!
ya askari trafik, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!
on Wednesday, September 19, 2012
Post a Comment