Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MZEE MWINYI AWAKABIDHI KWADELO TANGI LA MAJI, KITANDA CHA KUJIFUNGULIA


 Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omari Kariati akimsalimia Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwa Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi (kushoto), Mikocheni jijini Dar es Salaam. kabla ya hafla ya wananchi wa Kata hiyo kukabidhiwa tangi la maji na kidanda cha kujifungulia kina mama, iliyofanyika nyumbani hapo, leo.
 Diwani Kariati akiongozana na Mzee Mwinyi na Mama Sitti Mwinyi kwenda eneo la tukio
 UNAONA MAMBO YA KILIMO KWANZA? Akasema Omari Kariati wakati akitazama maembe yaliyopo kwenye mwembe wa kisasa uliopo nyumbani kwa Mzee Mwinyi.
 Kina mama wa Kwadelo wakiwa kwenye viwanja vya shughuli ya makabidhiano ya vifaa hivyo
 "Kwanza tunamshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mzee wetu  Ali Hassan Mwinyi kwa kutukaribisha nyumbani kwake kukamilisha hafla hii. Shughuli iliyotuleta hapa ni Mzee wetu kuwakabidhi wana-Kwadelo tangi kubwa la maji la sh. 650,000 na kitanda cha kujifungulia kina mama, kisha atamapatia sh. 200,000 kijana wetu aliyemuahidi kwa ajili ya kukamilisha masomo yake ya ualimu pale Ununio" akasema Diwani wa Kwadelo Omari Kariari kufungua shughuli. pembeni ni Mzee Mwinyi na Mkewe Mama Sitti, wakimsikiliza.
 Kisha mzee Mwinyi na mkewe wakasongea pamoja na waalikwa pahala vilipokuwa vitu vya kukabidhi. Hapa anakabidhi kitanda
 Kwa furaha baada ya kukabidhiwa, mama mmoja wa Kwadelo akakifanyia majaribio kidogo kitanda hicho.
 Kisha Mzee Mwinyi akakabidhi tangi la lita 5000 kwa Mwadham Msami (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kerereng'ombe, palepale Kwadelo. Naye Omari Kariati akishuhudia
 Baada ya kurejea meza kuu, Mzee Mwinyi akakabidhi sh. 200,000 kwa kijana, Kassim Omar kwa ajili ya kumalizia masomo yake ya ualimu Chuo cha Ununio, Bagamoyo.
 Kisha Mzee Mwinyi akaeleza yake ya moyoni kuwahusia wana Kwadelo na Watanzania kwa jumla akisema "wanaodhani maandamano yanaleta maendeleo wanapotea, maendeleo yanaletwa na kujituma na kutumia fursa zilizopo kufanya kazi kwa bidiii". Kushoto ni Mama Sitti Mwinyi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top