MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na nchi Kavu (SUMATRA),
imecharuka na kulitoza faini ya sh 250,000 basi la Kampuni ya Alsaedy
lenye namba za usajili T 327 BDP linalofanya safari zake kati ya Dar es
Salaam na Dodoma baada ya kuwatoza abiria nauli kinyume na sheria.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo (UBT), mmoja wa wakaguzi wa mabasi katika kituo hicho, Omary Salehe alisema kuwa nauli kwa mabasi yaendayo Dodoma ni sh 13,000, lakini kondakta wa basi hilo aliwatoza abiria nauli ya sh 20,000.
Salehe alisema baada ya kuthibitika kwa tukio hilo, walilitoza faini basi hilo na kumuamuru kondakta kuwarudishia pesa abiria.
Mmoja wa abiria katika basi hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Seif, alisema kuwa kondakta wa basi hilo aliwatoza abiria nauli hiyo, huku tiketi zikiwa hazioneshi kiasi cha nauli halisi waliyolipa.
CHANZO: TANZANIA DAIMA Msimamizi wa magari ya kampuni hiyo akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake, katika hali ya kujitetea alisema kuwa haoni kama Sumatra ipo makini na wajibu wake wa kukagua magari kama ilivyo ada.
“Kwa nini wasiwepo kila siku, ila wanakuja siku wanajua kuwa ni za wanafunzi, lazima nauli ipandishwe,” alisema.

Post a Comment