Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza kwenye kikao na ujumbe kutoka kampuni ya China National Gold Group Corporation. Ujumbe huo uliongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo, Bwana Song Xin Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Bwana Eric Shitindi na Kamishna Msaidizi wa Kazi, Bwana Josephat Lugakingira. Kampuni hiyo inataka kuwekeza nchini kwenye madini.
Kampuni ya “China National Gold Group Corporation” inayomilikiwa na Serikali ya China ilianzishwa mwaka 2002. Kampuni hiyo inajihusisha na utafutaji, uchimbaji na utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na madini. Katika mazungumzo yaliyofanyika tarehe 27/9/2012 katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya Wizara ya Kazi na Ajira, kampuni hiyo imeonesha nia ya kuwekeza nchini katika sekta ya madini. Aidha, ujio wa kampuni hiyo wizarani ni kujifunza sheria na kanuni za masuala ya kazi na ajira hapa nchini.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Dkt. Makongoro Mahanga akiwa kwenye kikao na ujumbe kutoka kampuni ya “China National Gold Group Corporation”. Ujumbe huo uliongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo, Bwana Song Xin. Kampuni hiyo inataka kuwekeza nchini kwenye sekta ya madini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kazi na Ajira
on Friday, September 28, 2012
Post a Comment