………………………………………….
Viongozi wa Baraza la
Vijana Chadema Bavicha wametakiwa kuwa tayari kusimamia miiko na sera za
chama cha Demokrasia na Maendeleo ili waweze kuwasaidia Wananchi wa
Tanzania ambao wamekosa matumaini kutokana na sera mbaya za Chama cha
Mapinduzi ambazo zimeshindwa kuleta msaada kwa Wananchi kwa miaka hamisini toka Tanzania ipate uhuru.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa
Bavicha Taifa Mheshimiwa Rafiki Lufunga ambaye alikuwa Mgeni rasmi
katika kufungua mafunzo kwa wa Viongozi wa Bavicha Mkoa wa ili kuwapa
uwezo na uelewe jinsi gani waweze kuwasidia Watanzani wote ambao wana
mahitaji mengi ambayo hayajatekelezwa ili kuwafanya waishi maisha
mazuri.
Amesema Viongozi wa Chadema
Wamefanya mambo mengi mazuri na wengine wao wanazidi kuwa wazee hivyo
Vijana wasioandaliwa vizuri watashindwa kuleta msaada kwa Watanzania
ambao wako njia panda kutokana na utawala ulioko madarakani kushindwa
kabisa.
Mwezeshaji wa Semina hiyo
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Chadema Mzee Silvesta Masinde
amesema semina hii imeshafanyika katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania na
sasa ni zamu ya Mkoa wa Mwanza na Wilaya zake zote, na kuongea kuwa
wanachofanya Chadema ni kuwaimarisha Vijana maana wanaamini nguvu ya
Chadema iko kwa Wananchi ambao wengi ni Vijana.
Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa
Mwanza Revocatus Mukelebe Bonventura amesema kuwa wao kama Viongozi wa
Bavicha Mkoa wamejiandaa vyema kwa ajili ya Mafunzo hayo na kusema kuwa
mafunzo hayo yatawaongezea uwepo wa kujiamini pamoja na utendaji wao ili
kuwasaidia Watanzania wa rika mbalimbali.


Post a Comment