MWANASOKA wa
zamani wa kimataifa wa Senegal, El Hadji Diouf ameanzisha vita ya maneno na
Steven Gerrard - akidai kwamba Nahodha huyo wa Liverpool ni
mbinafsi.
Diouf
amekuwa akikutwa na kasumba ya ukorofi katika klabu anayochezea na mshambuliaji
huyo mtukutu sasa asahau kabisa kurejea Anfield.
Akiwa Leeds
hivi sasa, mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 31 alichezea Wekundu hao kati ya
mwaka 2002 na 2004.
El Hadji Diouf
amemfungulia mdomo Steven Gerrard
"Gerrard
alikuwa ananionea wivu wakati huo natikisa ulimwengu wa soka. Hakukuwa na
mbinafsi zaidi yake... hajali kuhusu mtu yeyote.
"Gerrard
yuko tayari Liverpool ifungwe, lakini yeye amefunga bao. Wakubwa wa Liverpool
hawana cha kusema juu yake. Sikuweza hata kuanzishwa na [Jamie]
Carragher."alisema.
Akiwa
Liverpool, Diouf alifungiwa na kutozwa faini kwa kugombana na shabiki wa Celtic
katika mechi ya Kombe la UEFA Uwanja wa Parkhead.
Nahodha wa Liverpool,
Gerrard amepewa makavu na Diouf
Diouf sasa
anajipanga upya kisoka akiwa Nahodha wa Leeds inayocheza Daraja la Kwanza, chini
ya kocha Neil Warnock.
Klabu
nyingine alizochezea ni Sochaux, Rennes, Lens za Ufaransa, Bolton, Sunderland,
Blackburn za England, Rangers and Doncaster za Scotland lakini licha ya utukutu
wake, hakuna shaka juu ya uwezo wake uwanjani.
"Siku moja
nilikodi ndege na Maradona. Akanishika mkono na kusema anafurahia kuniona
nacheza. Hiyo ilinifurahisha."alisema Diouf.
Ameichezea
Senegal mechi 69 na amesema: "Rejea Senegal, mimi ni Mungu wao. Watu walifanya
fujo kwa sababu sikuitwa kucheza mechi ya mchujo na Ivory
Coast."alijigamba.
Diouf alikuwa mchezaji
mwenzake Gerrard Liverpool kati ya 2002 na 2004
Post a Comment