Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa
nyumbani kwa marehemu kijijini Kiwangwa,wilayani Bagamoyo leo jioni wakati Rais
Kikwete alipokwenda kushiriki mazishi ya Marehemu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika
kaburi la marehemu Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa wakati wa mazishi
yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu kijiji cha Kiwangwa wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani leo jioni.
Marehemu alifariki juzi tarehe 25 Oktoba nyumbani kwake Kijitonyama
jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda na ameacha mjane, watoto wanne na wajukuu watatu Picha na Freddy Maro.
Enzi za Uhai wake Marehemu Luteni Kanali Mtengwa
aliwahi kuwa mpambe wa Rais wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi,kuanzia mwaka
1995 hadi mwaka 1995.Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika Wizara ya Sheria
na kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya
jeshi.
Marehemu alifariki juzi tarehe 25 Oktoba nyumbani kwake Kijitonyama
jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda na ameacha mjane, watoto wanne na wajukuu watatu Picha na Freddy Maro.
Post a Comment