Kamanda mwanadamizi wa
Somalia ameuwawa alipoviziwa na kushambuliwa na kundi la wapiganaji wa Kiislamu,
Al Shabaab.
Gavana wa jimbo la
Shabelle Kusini, kusini mwa Somalia, alisema Jenerali Ibrahim Mohamed Farah
Gordon na wanajeshi wengine watatu waliuwawa karibu na mji wenye bandari, mji wa
Merca.
Al Shabaab - ambao
wanadhibiti eneo karibu lote la kusini na kati mwa Somalia - hivi karibuni
waliondoka katika miji yote mikubwa, pamoja na Merca.
Kundi hilo bado
linafanya mashambulio ya kuvizia na mengineyo.
Post a Comment