Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIMBUNGA CHA SANDY CHALETA VIFO NA MAAFA MAKUBWA MAREKANI


Kimbunga Sandy kikiendelea kupiga majiji nchini Marekani baada ya kutoka Carribean na kupiga Canada
Kimbunga Sandy kikiendelea kupiga majiji nchini Marekani baada ya kutoka Carribean na kupiga Canada.

KIMBUNGA kikali ambacho kimepiga nchini Marekani hasa upande wa Mashariki mwa Taifa hilo kinachotambulika kwa jina la Sandy kimesababisha vifo vya watu kumi na tatu huku melfu ya wananchi wakiendelea kuhama makazi yao kujiepusha na madhara ambayo yanaweza yakajitokeza.

Madhara ya kimbunga cha Sandy ambacho kinatajwa kutokea nchini Canada na kupiga maeneo ya Pwani ya Marekani licha ya kusababisha vifo lakini kimewaacha watu zaidi ya milioni tano na laki tano bila ya huduma ya nishati ya umeme kutokana na miundombinu yake kuharibiwa.

Kimbunga cha Sandy kimeenda sambamba na kumiminika kwa theluji kwenye maeneo mengi nchini Marekani kitu ambacho kimeongeza ugumu kwa wananchi ambao wanahama makazi yao kupisha madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokanana na kimbunga hicho.

Miundombinu ikiwa ile ya barabara imeharibiwa vibaya kutokana na maji kujaa kwenye majiji mbalimbali nchini Marekani huku serikali wa Washington ikiendelea kutoa tahadhari kwa wananchi kuondoka kwenye maeneo ambayo yapo karibu na Pwani.

Kimbunga Sandy kabla hakijapiga nchi za Canadana na Marekani tayari kilishasababisha vifo vya watu sitini na saba katika eneo la Carribbean na hofu imeongezeka nchini Marekani idadi ya vifo inaweza ikaongezeka kutokana na kutokea maporomoko.

Majiji ambayo yameathirika zaidi ya kimbunga cha Sandy ni pamoja na New York, New Jersey, Pennsylvania, Maryland, West Virginia na North Carolina ambapo Maofisa wameendelea kuwasihi wananchi kuondoka kwenye makazi yao.

Kimbunga hiki kimeathiri kampeni za uchaguzi wa urais nchini Marekani ambapo kwa mara ya pili Rais Barack Obama na hasimu wake Mitt Romney wamelazimika kusitisha harakati zao za kunadi sera zao kupisha watu kuondoka kwenye makazi yao.

Rais Obama naye ametumia fursa aliyoipata akiwa Washington kutoa wito kwa wananchi kutii amri ambazo zinatolewa na Mamlaka husika kuhusiana na taarifa za mwenendo wa kimbunga zinavyotolewa.

Shughuli nyingi zimetatizika ikiwemo kufungwa kwa shule na kuahirishwa kwa safari za ndege na reli kutokana na kujiepusha na madhara ambayo yanaweza kutokea kutokana na kuendelea kwa kimbunga cha Sandy.

Kimbunga cha Sandy kimesababisha vinu vya nyuklia vilivyopo New Jersey kuzingirwa na maji na tayari tahadhari imetolewa ya watu kukaa mbali kwani kama ikivuja isije ikaleta athari
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top