Hamdu zote ni za Allah,
Mola Mlezi wa viumbe pia. Na rehema za Allah na salamu Zake zimfikie Mtume
Mtukufu Mwaminifu na Aali zake watoharifu, wateule na masahaba wake
wema.
Msimu wa Hija uliojaa
rehema na baraka umewadia na kwa mara nyingine na watu waliofanikiwa kwenda
katika miadi hii iliyojaa nuru, wamo katika kumiminiwa baraka za Mwenyezi Mungu.
Hapa, ninatoa mwito kwenu nyote mahujaji kutumia fursa ya kuwepo mahala hapa na
kuwemo katika wakati huu, kujiimarisha kimaanawi na kimaada. Hapa, Waislamu
wanaume kwa wanawake wanaitikia labeka mlingano wa Mola wao Mkubwa wa kujipamba
kwa sifa na matendo mema; kwa nyoyo na midomo yao.
Hapa watu wote wanapata
fursa ya kufanya mazoezi ya kudumisha udugu, mshikamano na kujiepusha na maasi.
Hii ni kambi ya malezi na mafunzo, ni maonyesho ya umoja, adhama na jinsi umma
wa Uislamu ulivyokusanya pamoja sura za watu tofauti, ni kambi ya kupambana na
shetani na mataghuti. Hapa Mwenyezi Mungu Mwingi wa hekima na Muweza amepafanya
kuwa ni mahala ambapo waumini waweze kuona manufaa yao ndani yake.
Tutakapofungua macho yetu ya busara na ibra basi ahadi ya mbinguni itaweza
kuenea katika maisha yetu yote; ya kila mmoja wetu na ya jamii
nzima.
Sifa za kipekee za amali za
Hija ni kule kuchanganya kwake dunia na Akhera na kuchanganya kwake masuala ya
watu binafsi na ya kijamii. Al Kaaba isiyo na doa na iliyotukuka; kutufu miili
na nyoyo za watu katika mhimili mmoja madhubuti na wa milele; amali ya Sai
(baina ya Safa na Marwa) na kufanya jitihada za mfululizo na za mpangilio mmoja
kutoka nukta ya kuanzia hadi nukta ya kuishia; kugura mahujaji wote kuelekea
kwenye nyuga za ufufuo za Arafa na Mash’ar na shauku na uhudhurishaji wa moyo
katika Mash’ar na maqam hayo adhimu, huleta unyofu na hali mpya, mapambano ya
pamoja ya watu wote ya kukabiliana na vielelezo vya shetani, na hatimaye kwa
pamoja na kutoka kila mahala na kila rangi na kila namna; wote wanashiriki kwa
pamoja katika amali hizo tukufu zilizojaa neema na utukufu na zilizojaa maana na
ishara za uongofu. Sifa za kipekee za faradhi hii zimejaa maana na
madhumuni.
Ni amali kama hii ndiyo
ambayo inauunganisha moyo na kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na kuujaza nuru na
kuunawirisha upweke wa moyo wa mwanadamu kwa imani na taqwa na wakati huo huo
kumvua mwanadamu kutokana na mzingiro wa ubinafsi na kumsahilishia mambo katika
jamii iliyopambika kwa sura za kila namna, ya umma wa Kiislamu na kumvisha nguo
ya kujiepusha na madhambi ambayo huilinda roho yake kutokana na mashambulizi
yaliyojaa sumu ya mashambulizi na vile vile humuongezea nguvu na moyo wa
kupambana na mashetani na mataghuti. Ni mahala hapo ndipo ambapo hujaji
anapoweza kuonana na Waislamu wenzake wengi wanaunda umma mkubwa wa Kiislamu na
kuona kwa karibu nguvu na uwezo wa umma huo na hivyo kupata matumaini kuhusu
mustakbali mwema na vile vile kupata hisia za wajibu wa kutoa mchango wake wa
kuimarisha umma huo na pia kama atapata taufiki na msaada wa Mwenyezi Mungu
aweze kutoa bay’a na kutangaza utiifu wake kwa Mtume (Muhammad) Mtukufu wa
daraja na kufunga mithaki na ahadi imara kwa Uislamu azizi na kutia nia ya kweli
ya kuijenga kiimani nafsi yake, kuleta marekebisho katika umma na kutia nguvu
neno la Uislamu.
Mambo yote haya mawili,
yaani kuijenga nafsi na kuujenga umma (wa Kiislamu) ni faradhi zisizoishiwa na
wakati na wala zisizofungwa. Njia za kuweza kufanikisha faradhi hizo mbili si
nzito kwa watu wenye mazingatio na wanaoangalia mambo kwa kina katika
utekelezaji wa majukumu ya kidini na kutumia vizuri akili, tabasuri na wenye
mtazamo wa mbali.
Kujenga nafsi huanzia
kwenye kupambana na hisia za kishetani na kufanya juhudi za kujiepusha na
madhambi na kujenga umma huingia sura kwa kumjua adui na njama zake, kufanya
jitihada za kupelekea mashambulizi, hadaa na uadui wa maadui usiwe na athari
zozote na hadi kufikia kwenye kuziunganisha nyoyo na mikono pamoja na lugha za
matabaka yote ya Waislamu na mataifa yote ya Kiislamu.
Katika wakati huu tulio nao
hivi sasa, moja ya masuala muhimu zaidi ya umma wa Kiislamu ambalo lina
mfungamano (wa moja kwa moja) na mustakbali wa umma wa Kiislamu, ni matukio ya
mapinduzi katika nchi za kaskazini mwa Afrika na katika eneo la Mashariki ya
Kati ambayo hadi sasa yameshapelekea kuanguka tawala kadhaa fasidi na vibaraka
wa Marekani na waitifaki za Uzayuni na kuzitikisa tawala nyingine kama hizo.
Kama Waislamu watapoteza fursa hii adhimu na iwapo watashindwa kutumia fursa hii
katika kuujenga vizuri na kuleta marekebisho kwenye umma wa Kiislamu, basi
watakuwa wamepata hasara kubwa. Hivi sasa mabeberu wavamizi na waingiliaji wa
masuala ya ndani ya mataifa mengine wanafanya juhudi zao zote kujaribu kupotosha
harakati hizo adhimu za Kiislamu.
Katika harakati hizo kubwa,
Waislamu wake kwa waume wamesimama kupambana na ukandamizaji wa watawala (wao
madhalimu) na kupambana na udhibiti wa Marekani ambao umepelekea kudhalilishwa
na kudunishwa mataifa ya Waislamu na kusababisha kushuhudiwa ushirikiano baina
ya tawala za nchi hizo na utawala mtenda jinai wa Kizayuni. Waislamu wamegundua
kuwa kitu kinachoweza kuwaokoa katika mapambano haya ya kufa na kupona ni
Uislamu, mafundisho ya dini hiyo tukufu na nara na kaulimbiu zake zenye uwokovu
na hilo wamelitangaza wazi wazi. Ajenda yao kuu wameifanya kuwa ni kulitetea
taifa madhulumu la Palestina na kupambana na utawala ghasibu (wa Kizayuni).
Wamenyoosha mkono wa urafiki kwa mataifa yote ya Waislamu na wanataka kuona umma
wa Kiislamu unashikamana na kuwa kitu kimoja.
Hii ndiyo misingi mikuu ya
harakati za wananchi kwenye nchi ambazo katika kipindi cha miaka miwili
iliyopita, wananchi wake wamenyanyua bendera ya uhuru na mabadiliko na
kujitokeza kwa viwiliwili na roho zao kwenye medani za mapinduzi na ni mambo
kama haya ndiyo yanayoweza kuwa misingi mikuu ya kuleta marekebisho katika umma
mkubwa wa Kiislamu. Kusimama imara na kushikamana vilivyo na misingi mikuu ni
sharti la lazima la kuweza kupata ushindi wa mwisho wa harakati za wananchi
kwenye nchi hizo.
Lengo la adui ni kutaka
kuhakikisha anateteresha misingi hii mikuu. Mikono fasidi ya Marekani na NATO na
Uzayuni inatumia baadhi ya mighafala na mitazamo finyu kujaribu kupotosha wimbi
la harakati ya vijana Waislamu na wanatumia jina la Uislamu kuwagombanisha
Waislamu na wanaiita jihadi ya kupambana na ukoloni na Uzayuni kuwa ni ugaidi
usio na macho katika ulimwengu wa Kiislamu ili Waislamu wauane wao kwa wao na
hivyo maadui hao wa Uislamu waweze kuokoka na Uislamu na wanajihadi wake
watazamwe kwa sura mbaya na chafu.
Baada ya maadui kukata
tamaa kwa kuona kuwa hawawezi kuushinda Uislamu wala kuzima nara na kaulimbiu
zake, hivi sasa wameamua kuzusha fitna kati ya makundi tofauti ya Waislamu na
wanafanya njama za kueneza chuki dhidi ya Ushia na chuki dhidi ya Usuni ili
kuzuia kupatikana mshikamano na umoja katika umma wa
Kiislamu.
Maadui wanawatumia vibaraka
wao katika eneo (la Mashariki ya Kati), kuzusha mgogoro nchini Syria ili
kuzishughulisha akili za mataifa ya dunia na kuzifanya zisahau masuala muhimu ya
nchi zao na zisahau pia hatari zinazowakabili. Maadui hao wanajaribu
kuwashughulisha (Waislamu) na masuala ya umwagaji wa damu ambayo maadui
wameyazusha wao wenyewe. Vita vya ndani nchini Syria na kuuliwa vijana wa
Kiislamu kwa mikono ya Waislamu wenzao ni jinai ambazo zilianzishwa na Marekani
na Uzayuni na tawala tiifu kwa maadui ambazo wanazidi kuchochea moto huo. Nani
anaweza kuamini kuwa, tawala ambazo zilikuwa waungaji mkono wa madikteta waovu
wa Misri na Tunisia na Libya, hivi sasa wamekuwa waungaji mkono wa kutaka
demokrasia taifa la Syria? Kadhia ya Syria ni suala la kulipiza kisasi dhidi ya
utawala wa nchi hiyo ambao katika kipindi cha miongo mitatu ulikuwa umesimama
peke yake kupambana na Wazayuni maghasibu na kuyaunga mkono makundi ya
wanamuqawama wa Palestina na Lebanon.
Sisi tunaliunga mkono taifa
la Syria na tunapinga uchochezi na uingiliaji wa aina yoyote ile wa kigeni
nchini humo. Marekebisho ya aina yoyote ile nchini humo inabidi yafanywe na
wananchi wenyewe na kwa kutumia njia zinazokubaliwa kikamilifu na wananchi wa
taifa hilo. Hatua ya mabeberu wa kimataifa ambao kwa msaada wa tawala za
vibaraka wao katika eneo hili wanatumia kisingizio cha kuenea mgogoro na wakati
huo huo kutumia kisingizio cha kuweko mgogoro kuhalalisha kufanya kila aina ya
jinai nchini humo ni hatari kubwa ambayo kama tawala za eneo hili hazitajiepusha
nayo basi inabidi zisubiri zamu yao ifike ya kukumbwa na hadaa hizo za
kibeberu.
Makaka na madada! Msimu wa
Hija ni fursa ya kutaamali na kuyaangalia kwa kina masuala muhimu ya ulimwengu
wa Kiislamu. Hatima ya mapinduzi ya eneo hili na juhudi za madola makubwa
yaliyojeruhiwa kutokana na mapinduzi (ya wananchi wa eneo hili) za kutaka
kuyapotosha mapinduzi hayo ni miongoni mwa masuala hayo (muhimu ya ulimwengu wa
Kiislamu ambayo inabidi kuyaangalia kwa kina). Njama za wasaliti za kutaka
kuzusha hitilafu kati ya Waislamu na kuleta ugomvi na suutafahumu kati ya nchi
ambazo zimeamua kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu; kadhia ya Palestina na
juhudi za kuifanya itengwe na kuizima jihadi ya Wapalestina; propaganda za
kueneza chuki dhidi ya Uislamu zinazofanywa na tawala za Magharibi na uungaji
mkono wa tawala hizo kwa watu wanaomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW; kuandaa
mazingira ya kuzuka vita vya ndani na kugawanywa vipande vipande baadhi ya nchi
za Waislamu; kuzitisha tawala na wananchi wa nchi za Kiislamu zilizofanya
mapinduzi kuhusiana na hatari za kupinga siasa za kibeberu za Magharibi na
kueneza dhana potofu kuwa mustakbali wao unategemea kujisalimisha kwao mbele na
madola ya kibeberu na masuala mengine muhimu sana kama hayo, ni miongoni mwa
kadhia muhimu ambazo inabidi ziangaliwe kwa taamuli na kwa mazingatio makubwa
katika fursa inayopatikana kwenye Hija na chini ya kivuli ya kupendana na kuwa
na fikra moja nyinyi mahujaji.
Ni jambo lisilo na shaka
kwamba uongofu na msaada wa Mwenyezi Mungu utawaangazia njia za salama na amani
waumini wenye kufanya jitihada katika mambo yao, ?????? ?????? ???? ????????
?????Na wanaofanya juhudi kwa ajili Yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia Zetu. (al
Ankabut – 29:69).
Wassalaamu Alaykum
Warahmatullahi Wabarakaatuh.
Sayyid Ali
Khamenei,
Post a Comment