Serikali
imeboresha miundombinu ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja
na wilaya zake kwa kuwa na mtambo unaozalisha umeme mwingi kuzidi
mahitaji ya mikoa hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme TANESCO
Mkoa wa Mtwara Mhandisi Daniel Kiando alisema kwa sasa mtambo una uwezo
wa kuzalisha umeme wa megawati kumi na nane (18) wakati mahitaji ya
mikoa hiyo ni megawati kumi na tatu (13).
“Kwa
sasa mtambo wetu unazalisha umeme wa kutosha kiasi kwamba tuna ziada
ya umeme wa megawati tano, hata hivyo tunaendelea kuzalisha umeme
kulingana na mahitaji ya mikoa yetu,” alisema Kiando.
Kiando
amefafanua kuwa mtambo huo unaozalisha umeme kwa kutumia gesi
unasambaza umeme wa megawati 7.5 katika Mkoa wa Mtwara na megawati 5.5
katika Mkoa wa Lindi.
Kutokana
na uboreshaji huo, wananchi wa Mtwara na Lindi wamepata punguzo la
umeme ambapo kwa sasa wanalipia umeme kwa elfu tisini na tisa badala ya
laki nne na elfu hamsini na tano na mwisho wa punguzo hili ni mwezi
Desemba mwaka huu.
Mwezi
Aprili mwaka huu, Serikali iliamua kuchukua mtambo huo wa kuzalisha
umeme kutoka kwa wawekezaji wa Artmas na hivi sasa mtambo unazalisha
umeme kwa kutumia gesi badala ya mafuta mazito kama ilivyokuwa hapo
awali.
Post a Comment