Mrembo wa
Ilala, Magdalena Roy, usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kunyakua taji la
mrembo wa pili kuingia hatua ya nusu fainali ya Redd's Miss Tanzania
2012 baada ya kuwashinda warembo wengine 29 na kutwaa taji la Top Model.
Magdalena
aliibuka mshindi katika shindano dogo la Redd's Miss Tanzania
lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Kimataifa ya Naura
Springs jijini Arusha.
Kwa
matokeo hayo Top Model, Magadalena Roy anaungana na Miss Photogenic,
Lucy Stephano katika nusu fainali hiyo na kukaa tayari kusubiri warembo
wengine 13 watakaoungana katika Nusu fainali hizo.
Taji la TOP MODEL lilikuwa linashikiliwa na mrembo wa Temeke, Mwajabu Juma.
Mrembo
kutoka Mkoa wa Mara na Miss Kanda ya Ziwa 2012, Eugene Fabian nae
alifanikiwa kutwaa taji la Ubalozi wa Hotel ya Naura Spring ya jijini
Arusha.
Egene
alitangazwa kunyakua taji hilo usiku wa kuamkia leo wakati wa shindano
dogo la Redds Miss Tanzania 2012 la kumsaka Top Model ambaye pia
ataingia katika hatua ya 15 bora ya Shindano hilo la taifa la Miss
Tanzania. Awali taji la Balozi wa Naura Spring Hotel lilikuwa
likishikiliwa na Neema Joel.
Post a Comment