Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisoma Hotuba ya kufunga
Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa aukifanyika katika
Ukumbi wake uliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Mh. Pandu Ameir Kificho akiwa na Makatibu wake wakitoka
nje ya Ukumbi wa Baraza hilo baada ya kuahirisha Kikao cha Baraza hilo Mbweni
nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mwakilishi wa
Jimbo la Kikwajuni Mh. Mahmoud Mohammed Mussa mara baada ya kubaliza Hotuba yake
ya kufunga mkutano wa Tisa wa Baraza la Wawakilishi
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Mohd Raza
Hassan akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi mara baada ya kufungwa kwa mkutano wa Tisa wa Baraza la Wawakilishi
Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
**************
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar haitamuonea haya wala kumuogopa mtu ye yote ambae
atabainika kuhusika na uvunjifu wa amani baada ya Seriikali kuvumilia vya
kutosha, uvumilivu ambao umefikia kikomo.
Kauli hiyo
imetolea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati
akiufunga mkutano wa Tisa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
uliokuwa ukifanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif
alisema Serikali kupitia vyombo vya ulinzi itaendelea kuvisaka vikundi vya
kihuni vinavyoendesha vitendo vya kuwatisha Wananchi na kuwanyang’anya vitu na
mali zao, kuchoma moto baadhi ya Majengo sambamba na kuharibu miundo mbinu ya
Bara bara.
Alisema
hali hiyo ya vurugu sio Utamaduni wa Wananchi wa Visiwa hivyi ambayo ni
ya kusikitisha iliyopelekea wananchi kuacha shughuli zao za kujitafutia riziki
kutokana na kusimama kwa harakati zao za
maendeleo
“ Tutafanya
kosa kubwa sana ikiwa tutaanza kuichezea amani tuliyonayo kwani
kuvunjika kwa amani Nchini mwetu ndio chanzo cha kuvunjika kwa Umoja wetu.”
Alisisitiza Balozi Seif.
Aliwanasihi
Wananchi kuacha kujiingiza katika vitendo vya uvunjifu wa amani kwani kutenda
hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria na Serikali haitasita kumchukulia hatua mtu
ye yote atakayejihusisha na vitendo hivyo.
Aidha Balozi Seif
aliwaomba Wananchi kutoa Taarifa kwa vyombo vya dola mara tu watakapoona dalili
za watu wenye nia ya kutaka kufanya vitendo vya uvunjifu wa
amani.
Akizungumzia
suala la Rushwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali
inaendelea kuchukuwa hatua za kuimarisha Taasisi za kupambana na
Rushwa.
Alisema Viongozi
pamoja na Wananchi wana wajibu wa kutoa ushirikiano kwa Taasisi ya
kupambana na Rushwa iliyopitishwa na Baraza hilo hivi karibuni ili iweze
kutekeleza majukumu na wajibu wake kwa mujibu wa sheria na kwa kwa
faida ya maendeleo ya Taifa.
“ Kama sote
tunavyojua rushwa ni adui wa haki na hivyo haina budi kupigwa vita ili
itokomezwe kabisa. Lakini hizi hazitafanikiwa bila ya ushirikiano wa wananchi
wenyewe”. Alifafanua Balozi Seif.
Kuhusu kundi la
watu wenye Ulemavu Balozi Seif alisema Serikali imeweka mikakati katika kujenga
usawa na kuheshimu haki za watu wote wenye
ulemavu.
Alieleza kwamba
kuwapatia watu wenye nulemavu haki zao za msingi ni jambo la Kikatiba na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha azma hii inafikia malengo
yaliyowekwa.
Balozi Seif
aliipongeza Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa juhudi kubwa
inayochukuwa katika kuimarisha mazingira kwa watu wenye ulemavu na kuwajengea
uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya Kijamii na
Kiuchumi.
Akigusia suala la
tume ya kukusanya na kuratibu Maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Muungano Balozi
Seif aliwaomba Wananchi ambao bado hawajatoa maoni yao kuitumia fursa hiyo
itakayoamua mambo muhimu yatakayokuwa na maslahi kwa Jamii
yetu.
Alisema si vyema
kwa baadhi ya vikundi vya Wananchi kuiacha fursa hii na kuendelea kutoa matamshi
yanayochochea nchuki, uhasama na vurugu kwa kisingizio cha kuukataa
Muungano.
ASlisisitiza
kwamba jambo la kubwa la kuzingatia ni kuitumia fursa hii ili
Wananchi wote waweze kuitoa maoni yao kwa uhuru bila ya kubughudhiwa na
kutishiwa maisha yao.
Kuhusu Sekta ya
Umeme Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema suala la mgao wa
umeme karibu litakuwa historia katika Kisiwa cha Unguja kufuatia kutandikwa kwa
waya mpya wa umeme wenye uwezo wa kuchukuwa umeme wa Mega Watts 100 kazi ambayo
inatarajiwa kukamilika mwezi Disema mwaka huu wa
2012.
Alisema hatua hii
ni faraja kubwa kwa Wananchi wa Zanzibar hasa ikizingatiwa kwamba umeme ndio
nishati muhimu kwa shughuli za uzalishaji na maendeleo ya Taifa
hili.
Aliwataka
Wananchi wote waendelee kuitumia nishati ya umeme kwa shughuli zao za kujiajiri
kwa nia ya kujikomboa kutoka kwenye umaskini.
Baraza la
Wawakilishi Zanzibar limeahirishwa hadi jumatano ya Tarehe 16
Januari mwaka 2013 saa 3.00 za Asubuhi.
Na
Othman
Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
Post a Comment