Ili kuonyesha nia ya kutaka watoto
wake sita waweze kusoma na kufikia hatua nzuri ya kupata elimu ya Juu,
tayari Mama huyu, ambaye jina halisi ni Agness King'ombe, ambaye
alibadili dini na kuitwa jina la kiislam, Sada Masoud, anayewaacha watu
wengi na maswali yasiyokuwa na majibu pindi wanapomuona akiwa katika
maeneo yake ya makazi eneo ya Ufukwe wa bahari ya Hindi pande za Ocean
Road, amekwishaanza kuwafundisha na kuwapa elimu ya awali watoto wake
wa5, wenye umri wa kuanza masomo ya darasa la kwanza huku mtoto wake wa
kwanza mwenye umri wa miaka 12, Dyana Sailas, alitakuwa kuwa darasa la
Sita kwa sasa.
Je, wajua ni kwa nini Mama huyu alibadili dini na kuwa Muislam na kutumia jina hilo la Sada? kaa nami, katika ukurasa huu.
Sada, alisema kuwa, maisha anayoishi si
kwamba anapenda kuishi katika staili hiyo, la hasha, bali ni sehemu tu
ya maisha na staili ya masiha ya kiafrika iliyompelekea kuwa katika hali
hiyo na kujikuta kila mtoto anakuwa na baba yake.
Aidha, sada alisema kuwa amekuwa
akipata msaada wa kuwalea watoto wake kutoka kwa baadhi ya baba wa
watoto wake wanaomkumbuka siku moja moja, na kuamua kutumia sehemu ya
msaada huo kuwanunulia watoto chakula, nguo na vifaa vya kuwafundishia
watoto hao iki ni pamoja na Unifomu, Ubao, chaki, Vitabu na madaftari.
''Nimeamua kuwaandaa watoto wangu kwa
kuwafundisha kusoma na kuandika, na pia nawafundisha masomo ya
Kiswaahili, Kiingereza na Hesabu, ili kuwaandaa waweze kujua vyema ili
atakapojitokeza mfadhili wa kunisaidia niweze kuwapeleka kuanza shule
mwakani, na naamini hata walimu hawatapata shida katika kuanza nao kwani
tayari wanaweza kusoma na kuandika vizuri tu,
Huyu wa kwanza Dyana, kwa sasa
alitakiwa awe tayari yupo darasa la Sita lakini kutokana na sababu
zilizo nje ya uwezo wangu, nilishindwa kumpeleka kuanza shule hadi sasa,
lakini si haba nikipata mfadhili hata naye pia itabidi aanze tu la
kwanza''. alisema Sada.
Akielezea staili ya maisha yake
katika eneo hilo, sada alisema kuwa ikitokea siku amebahatika kupata
fedha za kutosha hujitahidi kukodi Hoteli ya bei nafuu na kulala na
watoto wake, na pindi anapokosa huwa tayari ameshajiandaa ambapo hutumia
Hema maalum ambalo hulijenga nyuma ya Hoteli ya Serena na kutumia
magodoro ya kujaza na kufunga Neti kubwa na kisha kuuchapa usingizi na
wanawe na kisha kuondoa asubuhi.
''Nimeamua kuchagua eneo hili la
chini ya mti kuwa makazi yangu na kama ofisi yangu nikiwa kama mwalimu
wa watoto wangu na pia nikiwa kama mfanyakazi wa watoto wangu, kwa
sababu eneo hili wanangu hupata maji kwa urahisi tu hapoa Gymkhana kwa
ajili ya kuwafulia nguo zao na kuwapikia chai ili wanywe kabla ya kuanza
vipindi kuwafundisha.
Na ninapofika hapa asubuhi baada ya
kuamka, kuwaandalia chai kwanza wanangu na kuwaogesha na kuwavisha
Unifom na baada ya kunywa chai hukaa kama hivyo kwenye mkeka kama
unavyowaona wakinisubiri nimalize kazi zangu ili tuanze darasa''.
alisema Sada
ZIJUE SABABU ZA MAMA HUYU KUBADILI DINI
''Sababu za mimi kubadili dini ni
kwamba, hivi sasa nina watoto Sita, ambao kila mmoja ana baba yake, na
baba mmoja kati ya hao sita alinidanganya nibadili dini ili aweze kunioa
na tuishi pamoja, lakini mwisho wa siku akanitelekeza na kunikimbia
hadi leo sijawahi kumuona tena baada ya kuniachaia mtoto''. alisema Sada
Sada
aliwataja kwa majina watoto wake kuwa ni, Dyana Silas, Michael Willson,
Junior Jonathan, Godlisa Carlos, Gudluck Alex na Trywell Jumpo, ambao
wote anaishi nao katika mazingira hayo magumu.
Watoto wa Bi. Sada, wakiwa darasani
wakimsubiri mwalimu Mama yao kuanza kuwafundisha leo asubuhi, huku
wakiwa katika sare za shule.
Bi Sada, akiwa bize kumalizia kazi
zake za kuosha vyombo baada ya kumaliza kunywa chai na kuwaogesha
watoto, wake ambao ni wanafunzi wake pia.
Wanafunzi hao wakijisomea, wakati wakimsubiri mwalimu wao...(kushoto) ni mtoto wake mdogo yeye akicheza tu...
Wanafunzi hao wakijisomea, wakati wakimsubiri mwalimu wao...
Hii ni sehemu ya kwanza, endelea kufuatilia mahojiano haya katika mtandao huu wiki ijayo, Sababu za kuachwa na kila mwanaume.
chanzo: Sufiani Mafoto
Post a Comment