……………………………………
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na
Ajira, Bwana Eric Shitindi amewahimiza Maofisa Kazi Wafawidhi nchini
kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kanuni za masuala ya
kazi.
Bwana Shitindi aliyasema hayo leo
katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao kazi cha Maofisa Kazi Wafawidhi
kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kazi na Ajira jijini Dar
es Salaam tarehe 4/10/2012.
Bwana Shitindi aliwaeleza Maofisa
Kazi Wafawidhi hao kutoka ofisi za Idara ya Kazi kote nchini kwamba
wana jukumu kubwa la kujenga na kuimarisha usalama na mahusiano mema
sehemu za kazi.
Kikao cha Maofisa Kazi hao
kinafanyika kwa siku mbili kikiwa na lengo la kutathmini utendaji kazi
wa Idara ya Kazi kwa mwaka uliopita pamoja na kujiwekea mikakati na
malengo kwa mwaka ujao.
Kikao hiki kitajadili hali ya
mahusiano sehemu za kazi nchini na mwelekeo wake pamoja na taarifa ya
ukaguzi wa shughuli za Idara vituoni.
Akimkaribisha Katibu Mkuu wizara
ya Kazi na Ajira kufungua rasmi kikao hicho, Kamishna wa Kazi, Bwana
Saul Kinemela alisema kuwa vikao kazi ni mfumo waliojiwekea Maofisa Kazi
kukutana kadri inavyowezekana ili kupitia, kujadili na kupanga mikakati
ya utekelezaji wa kazi zao.
Imetolewa na Ridhiwan Wema
MSEMAJI-WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Post a Comment