Kamishna kutoka Tume ya
Kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya nchini Bw. Christopher Shekiondo akizindua
rasmi maonyesho ya sanaa ya Sober House jijini Dar amesema kwa niaba ya tume ya
kudhibiti dawa hizo Zanzibar na kwa Serikali kwa ujumla wanatambua mchango wa
wadau mbalimbali uliosaidia vijana kuachana na tabia hiyo na kuahidi
kushirikiana nao katika kuhakukikisha asilimia kubwa ya vijana wanabadilika kwa
kutumia njia mbalimbali ikiwemo sera madhubuti za Serikali na mipango mikakati
ikiwemo utekelezaji wa Kampeni za ufahamu wa madhara ya madawa
hayo.
Ameongeza kusema kuwa
mikakati ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya inakabiliana na changamoto
nyingi kutokana na uhaba wa vituo na wataalamu lakini Serikali haijakata tamaa
na inaahidi kutimiza lengo hilo katika muda muafaka ikishirikiana na wadau
mbalimbali na kuomba wadau wengine wajitokeze.
Mkurugenzi wa Alliance
Francaise Tanzania Bw. Sullivan Benetier akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni
rasmi katika uzinduzi wa maonyesho ya sanaa ya Sober House Zanzibar ambapo
amesema wao wamekuwa wadau wakubwa wa kusaidia mpango wa kuwawezesha vijana
kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na kujirudi na kutumia vipaji
walivyonavyo kufanikisha maisha yao na kujipatia kipato.
Baada ya kufanikiwa kwa
mpango wa kuwawezesha watu wenye ulemavu wa ngozi sasa wamejikita katika
kuhakikisha vijana Tanzania wanaachana kabisa na wimbi la matumizi ya dawa za
kulevya kwa kuunga mkono shughuli hii ambapo vijana walioonyesha mfano kwa
kubadili tabia wanapata fursa ya kuonyesha sanaa zao za kuchora na kuchonga na
pia kutokuwa na vipindi vingine vya kutoa ushauri nasaha wa kiakili
utakowasaidia kujitambua na kuwafanya kuwa mabalozi watakaoelimusha vijana
wenzao kuachana na tabia za matumzi ya dawa hizo.
Mgeni rasmi katika
maonyesho ya Sanaa ya ‘Sober House’ yaliyozinduliwa jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya visiwani Zanzibar Dkt. Shekiondo
(wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wadau wanaondesha mkakati wa
kuwasaidia vijana kubadili tabia na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na
badala yale kuonyesha vipaji walivyo navyo katika sanaa.
Muasisi wa Sober House
Visiwani Zanzibar Bw. Suleiman Maulid akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake
ambapo ametoa wito kwa vijana wote Tanzania wanaojihusisha na utumiaji wa dawa
za kulevya kuachana na tabia hiyo na kisha kujiunga na Sober House kwa msaada
zaidi wa kimawazo, kifikra na kielimu. Pia ameitaka Serikali kuongeza nguvu
zaidi kwa taasisi zinazopambana na dawa za kulevya nchini katika kuwawezesha
kufanikisha mipango ya kuwawezesha vijana kujirudi.
Mkurugenzi wa Chama cha
maafisa Ustawi wa Jamii Bi. Anna Swai akionyesha Sanamu ya Msanii Mkongwe
nchini Bi. Kidude iliyotengenezwa na mmoja wa vijana waliobadili muelekeo na
kuamua kuachana na dawa za kulevya Zakaria Mwiru (kushoto) wakati wa ufunguzi wa
kazi za sanaa
Baadhi ya Wageni waalikwa
wakifuatilia uzinduzi wa Maonyesho ya Sanaa ya Sober House Recovery
yanayoendelea katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar na kiingilio ni
Bure kwa wote.
Raia wa kigeni akitazama
bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na vijana waliobadilika na kuamua kuacha
tabia za utumiaji wa madawa ya Kulevya na kujishughulisha na
sanaa.
Mbunifu wa Mavazi nchini na
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House (TMH) Khadija Mwanamboka a.k.a Kubwa la
Maadui alikuwa ni miongoni mwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho
hayo.Pichani akipozi na moja ya mkoba uliosukwa na mkeka ikiwa ni kazi za vijana
waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya na kujifunza fani mbalimbali na mwishowe
kuvionyesha kwa jamii.
Khadija Mwanamboka
akichukua taswira katika moja ya picha zilizoonekana kumvutia wakati wa
maonyesho ya Sober House Art Exhibition yanayoendelea katika Ukumbi wa Utamaduni
wa Ufaransa Alliance Francaise wa jijini Dar.
Maonyesho haya ni bure,
Tujitokeze kuwaunga vijana wetu walioamua kubadili tabia na tujifunze kutoka
kwao. “Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana”.
Kijana Zakaria Mwiru
akionyesha ubunifu wake wa kinyago chenye taswira ya Msanii maarufu wa muziki wa
taarab hapa nchini Bikidude ambayo ilimchukua muda wa wiki moja kutengeneza na
alifanya hivyo kutokana na kuvutiwa na kazi za muziki za msanii huyo
zilizoenea kote visiwani Zanzibar na kuamua kuchonga kinyago hicho. Kinyago
hichi kilianza kupigwa mnada kwa Dola 550 mwenye kuvutiwa nacho
ajitokeze.
Kazi ya mikono ya Zakaria
Mwiru. Pichani ni Sanamu ya Bi.Kidude.
Pichani Juu na Chini ni
kazi za Ubunifu zilizofanywa na Vijana waliobadili mwelekeo wa maisha waliopo
katika taasisi ya Sober House ya visiwani Zanzibar.
Kamishna kutoka
Tume ya Kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya nchini Bw. Christopher
Shekiondo (kushoto) akionekana kuvutiwa na moja ya sanamu ilyotengenezwa na
vijana waliobadili mwelekeo na kuamua kuachana na dawa za kulevya na kuendeleza
vipaji vyao ikiwemo sanaa ya uchongaji. Ahmed Awadhi
Mkurugenzi wa Alliance
Francaise Tanzania Bw. Sullivan Benetier (kulia) akibadilishana mawazo na
Mbunifu wa Mavazi nchini ambaye pia Balozi wa Sober House visiwani Zanzibar
Ally Rehmtullah (katikati) pamoja na Mwasisi na CEO wa Missie Popular Blog
Mariam Ndabagenga.
Post a Comment