KATIKA uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya daraja mbili Mkoani Arusha,Chama cha demokrasia na maendeleo chadema kimeibuka kidedea kwa kura 2047,CCM 1214,Cuf 162,Tlp,31,Nccr 18 hivyo mgombea udiwani wa chadema Prosper Msofe kupeperusha pendera katika kata hiyo
Hali
ilikuwa tofauti Wilayani Arumeru Mashariki ambapo chama cha CCM katika kata ya
bang”ata ilipeperusha vyema pendera yeke kwa kushinda kwa kishindo kikubwa kwa
kupata kura 1177,chadema 881 na Tlp kura 3
Uchaguzi
katika kata ya daraja mbili Arusha mjini ,msimamizi wa uchaguzi huo Omary
Mkombole alichelewa sana kutangaza matokeo hayo ya udiwani kwa kile
kilichoelezwa kuwa hakuwa na chombo chenyekuweza kuharakisha upatikanaji wa
matokeo hayo kwa haraka hali iliyosababisha matokeo hayo kutangazwa saa 4:30
usiku
Hata
hivyo katika uchaguzi huo vihoja vya hapa na pale viliibuka baada ya mgombea wa
CCM philip moshi kuingia mitini hata kabla ya matokeo hayo kutangazwa hali
iliyosababisha gumzo kubwa kwa wapiga kura
Hali
ya usalama uliimarishwa na jeshi la polisi huku wakiwa na silaha zao za
moto,mabomu,mbwa huku wananchi wakiwa wanaimba nyimbo za kila aina kama vile”ni
bora CCM kuliko ukwimu!!,Lowasa fisadi!!,Tunamtaka lema wetu na bila lema
patachimbika,, polisi ni wakwetuuuuuuu!!,,hizo baadhi tu ya nyimbo ambazo
walikwa wakiimba mashabiki wa chaema mbele ya polisi.
Kabla
ya matokeo hali ilikuwa hivi:
UCHAGUZI
mdogo wa udiwani katika kata ya Darajambili Mkoani Arusha tarehe 28 oktoba
mwaka huu, uliingia dosari baada ya risasi kurindima hewani mfulululizo hali
iliyozua taharuki kwa wakazi wa kata hiyo waliokuwa wamejitokeza katika vituo
vya kupigia kura.
Risasi
hizo zinadaiwa kupigwa na mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari
pamoja na mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM(Uvccm) wilayani Arusha,Godfrey
Mwalusamba mara baada ya kuibuka tafrani baina ya wafuasi wa CCM na Chadema
katika eneo la Shule ya sekondari ya Felix Mrema.
Katika
vurugu hizo dereva wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Haleluya Natai pamoja na
wafuasi wa Chadema zaidi ya 15 walikamatwa na jeshi la polisi huku Nasari na
aliyekua mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema wakitokomea kusikojulikana
lakini kisha baadaye walionekana katika viunga vya kupigia
kura.
Hatahivyo,katika
hali isiyo ya kawaida mgombea wa Chadema katika kata hiyo,Prosper Msofe
alionekana akirandaranda katika vituo vya kupigia kura huku akiwa na silaha yake
aina ya bastola kiunoni hali ambayo ilizua mshangao kwa wapiga kura wa kata
hiyo.
Katika
vurugu hizo inadaia kuwa Nasari aliyekuwa akiongozana na lema wakiwa katika gari
mojawapo walivamia ngome ya CCM iliyopo karibu na ofisi za chama hicho kata ya
daraja mbili hali ambayo ilipelekea wafuasi wa CCM kuwavamia lakini Nasari
alijiami na kasha kufyatua risasi tatu hewani.
Hatahivyo,kada
wa CCM ,Kabwelwa Mturuka alijeruhiwa mkononi kwa kukatwa na panga na watu
wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema wakati wa majibishano karibu na kituo
cha kupigia kura.
Katika
vurugu hizo mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha Martin Munis naye aliporwa simu
yake ya mkononi na fedha ambapo alitoa taarifa katika jeshi la polisi na kupewa
AR/RB/13624/2012 ya shambulio la kudhuru mwili dhidi ya Nasari na
Lema.
Wakati
huohuo,wafuasi wa Chadema waliokuwa mita chache karibu na kituo cha kupigia kura
cha sekondari ya Felix Mrema,walivamia ofisi za CCM zilizokuwa karibu na kituo
hicho na kisha kujaribu kung”oa bendera ya chama hicho lakini jitihada hizo
zilizimwa na wafuasi wa CCM baada ya kumshusha kabla hajaikaribia bendera
hiyo.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya matukio hayo
alisema kwamba ni mapema sana kuzizungumzia lakini alikiri kushikiliwa kwa
baadhi ya wafuasi wa CCM na Chadema ambao walihusika na vurugu katika uchaguzi
huo jana.
Kwa
upande wake,Nasari alipoulizwa juu ya hatua yake ya kurusha risasi hewani
alipinga vikali lakini alipotafutwa Mwalusamba alikiri kurusha risasi hizo
hewani huku akidai kwamba alifyatua kwa lengo la kujihami.
on Monday, October 29, 2012
Post a Comment