Alipotafutwa Tonya
Boy na kuzungumza juu ya ishu hiyo kuwa kulikoni hadi alilizwa kiasi hicho cha
pesa, ndipo alipodai kuwa kuna mmoja wa mademu wazuri wanaovuma kwenye tasnia
bongo movie ndiye aliyefanya mchezo huo mchafu kwani alijifanya anampenda sana
kumbe alikuwa anamuigizia na alikuwa na ishu yake.
Alidai kuwa baada ya tukio hilo
kutokeo demu huyo hakumuona tena na alikuja kusikia yupo mkoani kitu ambacho
kilimfanya aishiwe nguvu kwani hakuamini kilichotokea na hapo ndipo alipoamini
kuwa mademu wa tasnia hiyo ni wapigaji na ukiwaonesha kwako utajuta.
“Bongo movie hakuna demu yani
hata bure siwataki tena yani wanaleta maigizo hadi kwenye mapenzi dah kweli hii
tasnia ina laana na inahitaji kuombewa kwani wasanii wake wanatamaa ya hela na
wanamapepo ya ngono yani wakimuona mwanaume ana hela basi mate yanawatoka, hata
wa bure siwataki tena,” alidai.
Hata hivyo alipoulizwa jina la
msanii huyo wa filamu alishindwa kumtaja kwa madai kuwa hata kama aliiba kiasi
hicho cha pesa lakini kwa upande wake hana bifu naye ingawa hatamani hata
kumuona.
Post a Comment