Mtakatifu Tom katikati akisaini mkataba wa kuinoa Yemen na mabosi wake wapya (Picha zote kwa hisani ya Mtakatifu Tom) |
Na Bin Zubeiry
KOCHA
Mbelgiji Tom Saintfiet aliyefukuzwa Yanga baada ya siku 80 za kuwa kazini, jana
amesaini rasmi mkataba kuifundisha timu ya taifa ya Yemen katika sherehe
zilizoifanyika mjini Sana’a.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY kutoka Sana’a, Yemen jana, Mtakatifu Tom alisema amefurahia
mkataba huo mzuri na namna alivyopokewa kwa furaha na upendo katika ofisi mpya.
“Nimefurahi
sana, kila kitu ni kizuri, mazingira ya kufanyia kazi na watu waelewa pia, sasa
ni jukumu langu kuwafurahisha watu wa Yemen kwa kuwatengenezea timu nzuri
itakayowapa furaha kwa matokeo mazuri,”alisema Mtakatifu Tom.
Tom alisema
kwamba anatarajia kuiongoza timu hiyo ya Magharibi mwa bara Asia katika
michuano ya Kombe la Mataifa ya Magharibi mwa Asia (kama Kombe la Challenge la
CECAFA) itakayofanyika nchini Kuwait Desemba mwaka huu.
Alisema
katika michuano hiyo, amepangwa kundi moja na Saudi Arabia, Iran na Bahrain na
Januari mwakani, ataiongoza timu hiyo katika Kombe la Gulf huko Bahrain.
“Kwa sasa
nipo katika Jiji la Sana'a na kesho nitaanza kazi kwa kambi ya kujiandaa na
mchezo wa kirafiki Beirut, Oktoba 16 dhidi ya Lebanon,”alisema Mtakatifu Tom.
Saintfiet
alifukuzwa Yanga baada ya kutofautiana misimamo na uongozi wa Yanga, akiwa
amefanya kazi siku 80 na kuiachia timu taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, Kombe la Kagame.
Saintfiet
amefungwa mechi mbili Yanga katika mechi 14 alizoiongoza timu hiyo tangu
ajiunge nayo, Julai mwaka huu, akirithi mikoba ya Mserbia, Kostadin Bozidar
Papic.
Katika mechi
hizo, zimo sita za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame,
ambazo aliiwezesha Yanga kutwaa taji, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya Atletico
ya Burundi.
REKODI YA SAINTFIET YANGA
1.
Yanga
Vs JKT Ruvu (Kirafiki) 2-0
2.
Yanga
Vs Atletico (Burundi, Kagame) 0-2
3.
Yanga
Vs Waw Salam (Sudan, Kagame) 7-1
4.
Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 2-0
5.
Yanga
Vs Mafunzo (Z’bar, Kagame) 1-1
(5-3penalti)
6.
Yanga
Vs APR (Rwanda, Kagame) 1-0
7.
Yanga
Vs Azam (Kagame) 2-0
8.
Yanga
Vs African Lyon (Kirafiki) 4-0
9.
Yanga
Vs Rayon (Kirafiki, Rwanda) 2-0
10.
Yanga
Vs Polisi (Kirafiiki, Rwanda) 2-1
11.
Yanga
Vs Coastal Union (Kirafiki) 2-1
12.
Yanga
Vs Moro United (Kirafiki) 4-0
13.
Yanga
Vs Prisons (Ligi Kuu) 0-0
14.
Yanga
Vs Mtibwa (Ligi Kuu) 0-3
Post a Comment