MWANDISHI wa
habari mchunguzi wa Ugiriki amekamatwa kwa kuchapisha majina 2000 ya Wagiriki
wanaosemekana kuwa na akaunti za benki Uswiswi.
Orodha hiyo
ilipelekwa kwa serikali ya Ugiriki mwaka wa 2010 na waziri wa Ufaransa wa fedha
wakati huo, Christine Lagarde.
Shaka ilikuwa
watu hao waliweka fedha zao ng'ambo ili kukwepa kodi.
Lakini serikali
ya Ugiriki haikuchunguza watu hao kwenye orodha.
Orodha hiyo
inaitwa orodha ya "Lagarde:
jarida lenye
majina 2000 ya Wagiriki wenye akaunti katika benki ya HSBC mjini
Geneva.
Lakini mawaziri
wawili wa fedha wa Ugiriki wanashutumiwa kuwa waliificha orodha hiyo, na kuzusha
tetesi kwamba serikali imeshindwa kuchunguza kesi ambazo zinaweza kuwa za rushwa
kubwa.
Sasa mwandishi wa
habari maarufu wa Ugiriki, Kostas Vaxevanis, amekamatwa baada ya kuchapisha
orodha hiyo.
Anatarajiwa
kufikishwa mahakamani hapo kesho, kukabili mashtaka ya kufichua kitu cha
faragha.
Mwandishi huyo
anasema "badala ya kuwakamata wanaohepa kodi na mawaziri ambao walikuwa nayo
orodha, wanajaribu kukamata ukweli na uhuru wa vyombo vya habari."
Kati ya majina hayo kuna wanasiasa, wafanya biashara na wengineo, na imesababisha hamasa kati ya wananchi wa kawaida wa Ugiriki ambao wamezongwa na matatizo ya kiuchumi.
Na swala hilo
piya limezusha tena malalamiko kuwa kuhepa kodi nchini Ugiriki ni jambo
lilozagaa, na kwamba wakuu bado hawakushughulikia swala hilo
vilivyo.
Post a Comment