Pichani kulia ni Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumbaa akiyataja majina ya watuhumiwa hao wa mauaji ya Kamanda Barlo,na shoto ni IGP Said Mwema.
JESHI la Polisi
limewataja watuhumiwa 10, na bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine,
ambao inadai walishiriki kumuua aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza,
Liberatus Barlow.
Kati ya watu hao
watano wametiwa mbaroni Mwanza na watu watano kutoka Dar es
Salaam. Leo (jana) mjini Mwanza, mbele ya
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa makosa ya
Jinai Nchini (DCI) Robert Manumba aliwataja watuhumiwa hao ni Muganizi Michael
Peter (36) mkazi wa Isamilo ambaye inadaiwa alikiri mwenyewe kumuua kamanda kwa
risasi.
Wengine ni Chacha
Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward Kusota na Bhoke Mara Mwita
(42) ambao walikamatwa jijini Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego kwa msaada
wa wananchi.
Wanaoshikiliwa
jijini Mwanza kwa mahojiano ni pamoja na Mwalimu Doroth Moses Lyimo aliyekuwa na
RPC wakati mauaji yakitokea, Felix Felician Minde (50), Philemon Felician
(46) maarufu kama
Fumo, Bahati Agustino Lazaro (28) na Amos
Magoto (30) maarufu kama
Bonge.
Alisema
Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake Manumba kilijigawa kwenye
makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine la interejensia
huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya
simu.
Marehemu Kamanda
Barlow aliuawa usiku wa Oktoba 12 majira ya kati ya saa 7 na 8 usiku katika
eneo la Mianzi Mitatu, Kitangiri, kona ya Bwiru baada ya kupigwa risasi na watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu Dorothy
Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaa wa
Rufiji
Post a Comment