Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC CHIKU KUFUNGUA MASHINDANO HYA TAIFA CUP


Mama Chiku Gallawa

Na Mashaka Mhando, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mama Chiku Gallawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la Taifa ya mpira wa Kikapu, Taifa Cup mwaka 2012 yanayotarajiwa kuanza kesho kwenye viwanja vya Mkwakwani na Harbours Club vilivyo jijini Tanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanga (TRBA), Hamisi Jaffary alisema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na waamuzi kumi na mbili ambao watachezesha mashindano hayo tayari wameshawasili jijini hapa tokea mwishoni mwa wiki.
Jaffary alisema mashindano hayo yataanza Octoba 29 na kufikia tamati Novemba 5 mwaka huu na kushirikisha mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mpaka juzi mikoa kumi na sita ilikwisha kuthibitisha kushiriki mashindano hayo.
Mwenyekiti huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar ,Arusha,Moshi,Iringa, Mbeya,Mara, Lindi,Shinyanga,Tabora,Dodoma na Tanga ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo ambapo alisema timu nyengine huenda zitathibitisha katika shirikisho la mipira wa kikapu Taifa ikiwemo Zanzibar ,Unguja na Pemba.
Alisema mkoa wa Kigoma walijitoa dakika za mwishoni kushiriki mashindano hayo ambayo msimu huu idadi ya washiriki imeongezeka kutokana na kuongezwa kwa idadi ya mikoa.
Mashindano hayo wa mara ya kwanza yalifanyika jijini Tanga 1989 na mara ya mwisho ili kuwa ni 2005 msimu huu shamra shamra zimeonekana kuwa ni muda kubwa kutokana na kuwa maandalizi ya maandalizi yanayofanywa na mikoa shiriki huku viwanja ambazo zitatumika mashindano zimefanyiwa ukarabati wa hali ya juu.
Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa na wageni watapao 450 ikiwemo wachezaji na viongozi wa timu ambazo zitashiriki michuano hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo.
Aliongeza kuwa timu zilianza kuwasili jijini Tanga tokea Jumamosi na Jumapili ambapo kesho ndio ufunguzi rasmi wa mashindano hayo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top