Matokeo hayob yanaipeleka Dortmund kileleni mwa kundi
mbele ya timu ya Jose Mourinho, wakati City wanashika mkia wakiwa na pointi moja
tu baada ya kucheza mechi tatu.
Robert Lewandowski alifunga bao dakika ya 36, kabla ya
Cristiano Ronaldo kusawazisha ndani ya dakika mbili, lakini Marcel Schmelzer
akawafungia wenyeji la ushindi dakika ya 64.
Borussia Dortmund
wakishangilia kuifunga Real Madrid
Marcel Schmelzer akiifungia bao la ushindi
Dormund
Olympiacos walipata ushindi wa kwanza wakitoka nyuma na
kushinda 2-1 dhidi ya Montpellier nchini Ufaransa na kuongeza ugumu katika Kundi
B, baada ya Arsenal kufungwa na Schalke.
Gaetan Charbonnier aliifungia Montpellier dakika ya
49kabla ya Vassilas Torosidis kusawazisha dakika ya 73 na Kostas Mitroglou
aliyetokea benchi akafunga la ushindi dakika za majeruhi.
Matokeo ya jana yanaipeleka Schalke kileleni kwa pointi
zake saba, wakiizidi moja The Gunners, na Olympiacos inakwenda nafasi ya tatu na
Montpellier inaburuza mkia.
Olympiakos wamejiweka
katika nafasi nzuri
Malaga imeendeleza wimbi la ushindi kileleni mwa Kundi
C baada ya kuifunga AC Milan 1-0 na sasa inaongoza kundi hilo kwa pointi tatu
zaidi. Joaquin ndiye aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 64 kwa pasi ya Manuel
Iturra.
Mechi nyingine ya Kundi C, Zenit St Petersburg
waliifunga 1-0 Anderlecht nchini Urusi.
Alexander Kerzhakov alifunga dakika ya 72 kwa mkwaju wa
penalti, baada ya Milan Jovanovic kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari na
Alexander Anyukov.
Katika Kundi A, Porto imeendeleza rekodi yake nzuri ya
asilimia 100 kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Dynamo Kiev nchini Ureno.
Wageni walisawazisha mara mbili kupitia kwa Oleg Gusev na Ideye Brown baada ya wenyeji kufunga kupitia kwa Silvestre Varela na Jackson Martinez, kabla ya Martinez kufunga la ushindi zikiwa zimesalia dakika 12.
Wageni walisawazisha mara mbili kupitia kwa Oleg Gusev na Ideye Brown baada ya wenyeji kufunga kupitia kwa Silvestre Varela na Jackson Martinez, kabla ya Martinez kufunga la ushindi zikiwa zimesalia dakika 12.
AC Milan walifungwa na Malaga ya
Hispania
Katika Kundi A, Paris St Germain ilikwea nafasi ya pili kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dinamo Zagreb nchini Croatia, Zlatan Ibrahimovic akifunga la kwanza dakika ya 32 na Jeremy Menez akafunga la pili kabla ya mapumziko.
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk


Post a Comment