Katibu wa Bunge, Dk.Thomas Kashililah, aliithibitishia NIPASHE jana kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mbunge wa Mlalo (CCM), Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi ,imekamilisha kazi yake ya uchunguzi na kuikabidhi ripoti kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Naye Ngwilizi alisema taarifa rasmi za ripoti hiyo zitapatikana baada ya kuwasilishwa Bungeni.
“Msiwe na haraka juu ya taarifa hiyo, mtapata taarifa bungeni,” alisema Ngwilizi.
Naye Naibu Spika, Job Ndungai, alisema kwa mujibu wa utaratibu baada ya kamati kuwasilisha ripoti kwa Spika, Kamati ya Uongozi ya Bunge itakaa kujadili na kama itaona kuna umuhimu ripoti hiyo itaingizwa kwenye ratiba ya vikao vya bunge ijadiliwe.
Mapema mwezi uliopita Ndugai akizungumza wakati wa kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV alisema wabunge waliotuhumiwa kwa rushwa wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini huenda wakakabiliwa na hatari ya kuvuliwa ubunge na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.
Wabunge hao wanaweza wakapoteza nyazifa zao ikiwa Kamati ndogo Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayochunguza sakata hilo itathibitisha kama ni kweli walipewa rushwa.
Alisema Kamati ndogo ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyoongozwa na Ngwilizi, inao uwezo wa kupendekeza kama wabunge hao wavuliwe nyazifa zao au washitakiwe mahakamani.
Wakati wa mkutano wa bunge la bajeti ya mwaka 2012/13, baadhi ya wabunge walidai kuwa kuna wenzao wamehongwa na kampuni za mafuta ili kushinikiza Waziri wa Nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu, Eliakim Maswi, wang’olewe katika nafasi zao kwa kukiuka Sheria ya Manunuzi wa Umma.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment