Roma amekuwa kati ya wasanii wanaotumia sana mitandao ya kijamii vizuri kwa kueleza yake ya moyoni pale anapokuwa na kitu cha kusema.
Kupitia akaunti yake ya facebook, Roma alikuwa na haya ya kusema kuhusu kile kilichotokea na kumfanya aperform chini ya kiwango chake huko Dodoma siku ya Ijumaa iliyopita.
"PAZIA LINAFICHA MENGI SANA!! WATU WASIOFAHAMU MUZIKI NDO WANAPEWA VITENGO MUHIMU KATIKA HII SANAA YETU...
FINALLY THEY DESTROY THE WHOLE
SYSTEM!! INAUMAJE YAANI..
.LAITI UKWELI UNGEPEWA NAFASI BASI
WATU WENGI SANA WANGEAIBIKA DUNIANI HUMU!!! POLE DJ CHOKA KWA KILICHOKUKUTA
DODOMA JANA KWENYE SHOW YA INTERCOLLEGE ROYAL VILLAGE PALE!!
SAMAHANI PIA WANA DODOMA KWA MIMI
KUPERFORM CHINI YA KIWANGO (NILILIONA HILO). NYUMA YA PAZIA KUNA MENGI SANA
MSIYOYAJUA (BACK STAGE).
DAKIKA CHACHE WAKATI MR BLU
ANAMALIZIA KUPERFORM THEN NIENDE MIMI KUMALIZA SHOW. HUKU NYUMA YA JUKWAA
KULITOKEA ZENGWE, KWAMBA DJ CHOKA AMBAYE SIKU ZOTE AMEKUWA NDIYE DJ WANGU COZ A
KNW WAT HE GAT!! WALIMKATALIA ASIPANDE NA MIMI NA BADALA YAKE NIPANDE MWENYEWE
NA DJ WAO, KWA SABABU AMBAZO HAWAKUZITOA(PENGINE NI SABABU BINAFSI) NA MKATABA
HAUKUSEMA HIVO!!
SIKUKUBALI HILI NA NDIPO HAPO WALIPO
NIVURUGA AKILI, TENA WAKASEMA KAMA HUTAKI ACHA KUFANYA SHOW, KIUKWELI NILIACHA
NA KUANZA KUSEPA NA KUELEKEA HOTEL(KAMA NI MBWAI MBWAI watanga
twasemaga)
KWA BUSARA ZA GODZILLA AKASHAURI
NISISEPE NIKUBALI KUFANYA!! MIMI SIKUKUBALI KUFANYA BILA CHOKA!! SAWA NAWEZA
FANYA SHOW NA DJ YEYOTE NA HUWA NAFANYAGA HIVO... BUT KWA HILI NILISHAWAMBIA
NAJA NA CHOKA NA WAKAKUBALI NA KUMUWEKA KWENYE BAJETI YAO!!
KWANINI WAKATAE MWISHONI!!!??
HATA D.N.A WALIMFANYIA HIVO NASIKIA
NA WAKAMWAMBIA APANDE BILA DJ WAKE. NA YEYE ALIKUBALI!! (HALIKUNIPENDEZA HILI
KWAKWELI)
THANX GOD NILIKAZA HADI WAKASANDA NA
NIKAPANDA NA CHOKA(NDIYO MAANA TULICHELEWA KUPANDA HADI WENGINE MKAANZA KUSEPA
SOORRY DODOMA).
LAKINI SIKUWA KWENYE MOOD POA KAMA
NILIYOKUJA NAYO WALIKUWA WAMESHANIKATA, SO NIKAPERFORM KIBWEGE
SANA.
.LAKINI NILIFANYA BUSARA KULIKO
NINGESEMA NISIFANYE KABISA...MAANA HAMJUI YANAYOTOKEA NYUMA YA PAZIA!!!
TUNAKUMBANA NA MITIHANI MINGI SANA
LAKINI TUNAIPIGA VITA...ILI TUMAINTAIN NAFASI TULIYOPO.
SIJUI KWANINI NAPATA VIKWAZO KTK SHOW
ZANGU ZA ROUND HII!!
MUNGU TUONGEZE IMANI NA NGUVU NA
HEKIMA NA BUSARA KATIKA KAZI ZA MIKONO YETU!!!
Post a Comment