Hatimaye
serikali imeamua kuwachukulia hatua za kisheria watu
wanaohujumu utekelezaji wa mradi wa maji wa kijiji cha Laroi kilichoko
katika kata ya Mateves Wilayani Arumeru.

Akitekeleza
zoezi hilo Afisa Tarafa ya Mukulat Isack Kaserian Maroseck
alitoa amri ya kukamatwa kwa mzee Rorian Mesheikini baada ya mzee huyo
anayetuhumiwa kuongoza mgomo huo wa uchangiaji wa mradi wa maji na
uharibifu wa miundombinu ya maji, kukaidi kuhudhuria kwenye kikao cha
mazungumzo na viongozi mbalimbali ngazi ya kata na tarafa ili kumaliza
mgogoro huo.

Mkutano
huo ulioitishwa na afisa tarafa hiyo kwa niaba ya mkuu wa
wilaya ya Arumeru Nyerembe Munassa Jana katika ofisi ya kijiji cha
Laroi kilimtaka mzee Mesheikini kuhudhuria mkutano huo ili kutoa
malalamiko yake juu ya mgomo huo wa kuchangia mradi wa maji utakaokuwa
ukombozi na msaada mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo lakini alikataa
ndipo Afisa huyo kutoa amri ya kwenda kukatwa kwa mzee huyo na polisi.

Aidha
mzee Mesheikini na mwenzake ambaye hakuweza kufahamika kwa
haraka walikamatwa na jeshi la polisi na kupelekwa katika kituo kidogo
cha polisi usa river huku wengine 12 wakiendelea kutafutwa kwa tuhuma
za kukaidi amri ya kikao cha tarehe 29 agost ya kwenda kurejesha
miundo mbinu yote ya maji waliyoharibu.

Isack
alisema kuwa Kikao hicho cha tarehe 29 kiliwahusisha polisi,
viongozi wa tarafa ya mukulat na kata zote za Tarafa hiyo, viongozi wa
mradi na wananchi wote kwa ujumla na kujadili msaada wa mradi huo
ambapo wote kwa pamoja walikubaliana kuwa wote waliohusika kuharibu
miundombinu hizo za maji warejeshe kwa gharama zao haraka iwezekanavyo
ili shirika liendelee kusambaza maji.

Awali
mgogoro uliibuka katika kijiji hicho baada ya kuletewa mradi
wa
maji uliojulikana kama Olmulo development Trust mwaka2003 ambapo
wananchi hao walitakiwa kuchangia shilingi kumi(10)kwa ndoo ya maji ya
lita ishirini ili kusaidia ukarabati wa mradi huo pindi miundo mbinu
yake itakapoharibika ua kuchakaa huku mradi huo ukilenga kusaidia
vijiji saba lakini baadhi ya wananchi wa kitongoji cha namba mbili
namba tatu walikaidi hilo wakiongozwa na mzee Mesheikini.

wakielezea madai ya kukataa kuchangia mradi huo, mzee
Mesheikini
alisema kuwa hawapo tayari kuchangia mradi huo kwani awali walikuwa
wakitumia maji ya mabomba yaliyowekwa na mkoloni hivyo walitaka
kuendeleza mabomba hayo kwa kuyarepea tu na siyo kuweka mapya.

Post a Comment