Gari la Polisi la pili
ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walishitakiwa kwa
makosa ya kufanya fujo na uchochezi likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi
kuja Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe.
Askari wa kikosi cha
kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika eneo la Mahakama ya Wilaya
Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa
mashitaka yao.
Mmoja kati ya Viongozi wa
UAMSHO Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea
Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao.
Kiongozi wa Jumuiya ya
UAMSHO Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakama
ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha
fujo na uchochezi.
Baadhi ya Wananchi
walioenda Mahakamani hapo kwenda kushuhudia kesi inayowakabili Viongozi wa
Jumuiya ya UAMSHO ambao walikosa dhamana na kurudishwa
Rumande.
Post a Comment