SIMBA SC inaondoka kwa basi lake
mchana huu kwenda Tanga, tayari kwa mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, dhidi ya wenyeji Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel
Kamwaga amewaambia Waandishi wa Habari mchana huu kwamba, katika safari hiyo
timu hiyo itawakosa nyota watano, Emanuel Okwi ambaye amekwenda kujiunga na
timu yake ya taifa, Uganda, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ anayesumbuliwa na Malaria,
Haruna Shamte, Hamadi Waziri na Komabil Keita ambao ni majeruhi.
Kamwaga alisema kwamba Mrisho Ngassa
aliyekuwa anaumwa Malaria amepona na yumo kwenye msafara wa mabingwa hao
watetezi wa Ligi Kuu unaokwenda Tanga kwa basi jipya la kisasa, walilopewa na
wadhamini wao, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Katika kujiandaa na mechi ya Tanga,
Simba jana ilicheza mechi ya kujipima nguvu na kuifunga Azam FC mabao 3-2
katika mchezo wa kirafiki uliofanyika asubuhi kwenye Uwanja wa Chamazi, maarufu
kama Azam Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Simba leo yalifungwa
Ramadhani Singano ‘Messi’, Uhuru Suleiman ‘Robinho’ na Daniel Akuffo, wakati ya
Azam yalifungwa na Jamil Mchauru na Khamis Mcha.
Hiyo ilikuwa mechi ya nne Azam
inafungwa na Simba msimu huu katika mechi tano walizokutana hadi sasa, baada ya
awali kufungwa kwa penalti kwenye fainali ya Kombe la Urafiki, kufuatia sare ya
2-2, kufungwa 2-1 kwenye Nusu Fainali ya BancABC Sup8R na 3-2 kwenye mechi ya
Ngao ya Jamii, wakati wao walishinda 3-1 dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi,
katika Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Azam na Simba zitakutana tena
katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mzunguko wa kwanza, Oktoba
27, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba ndio inaongoza Ligi Kuu, hadi
sasa ikiwa imeshinda mechi tano kati ya sita ilizocheza na moja tu imetoka sare,
hivyo kujikusanyia pointi 16, wakati Azam inashika nafasi ya pili ikizidiwa pointi
tatu, ingawa pia iko nyuma kwa mchezo
Post a Comment