Shambulizi dhidi ya kiwanda cha Sudan liliwaua watu
wawili.
SUDAN imesema kuwa inapanga kuishtaki Israel kwa Umoja
wa Mataifa kuhusiana na madai ya shambulizi dhidi ya kiwanda chake cha silaha
mjini Khartoum.
Balozi wa Sudan
katika Umoja wa Mataifa Daffa-Alla Elhag Ali Osman, amesema kuwa Israel imevamia
kiharamu anga zake mara tatu katika miaka ya hivi karibuni.
Sudan hata hivyo
bado haijatoa ushahidi wowote kuunga mkono madai yake na Israel nayo haijatoa
tamko lolote kuhusu madai hayo dhidi yake.
Duru nchini Sudan
zinasema kuwa kiwanda hicho kilimiaminika kuendeshwa na Iran.
Mwandishi wa BBC
w amaswala ya ulinzi anasema inaaminika kuwa kiwanda hicho kilikuwa kinatengeza
roketi na zana zengine kwa niaba ya Iran ili kuzipeleka kwa wapiganaji wa
Hamas.
Na kwa hivyo
Israel iliona umuhimu wa kusitisha shughuli za kiwanda hicho nchini Sudan badala
ya kuchukua hatua ambazo zingeudhi Misri.
Ingawa srael bado
haijatoa tamko lolote kuhusu madai ya Sudan, afisaa mmoja wa ulinzi aliambia
vyombo vya habari kuwa Sudan ni nchi hatari ya kigaidi.
''Serikali ya
Sudan inaungwa mkono na Iran na inatumiwa kama kivukio cha silaha kupitia Misri
na kuingia Hamas pamoja na kuyaendea makundi mengine ya kigaidi. '' alisema
afisaa huyo.
Mwezi Aprili
mwaka jana,Khartoum ilidai kuwa Israel ilihusika na shambulizi lengine la angani
dhidi yake ambalo liliwaua watu wawili karibu na mji wa Port Sudan.
Israel pia
ililaumiwa kwa shambulizi lengine dhidi ya msafara wa magari Kaskazini Mashariki
mwa Sudan mwaka 2009
Post a Comment