Makamu wa chuo cha VETA mkoani Singida,akizungumza muda mfupi kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa madereva wa magari ya abiria mkoani Singida.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa SUMATRA Bw. Ahmad Kilima akizungumza kwenye hafla ya kufungua mkutano wa madereva wa magari ya abiria mkoani Singida.Mkutano huo uliofanikiwa ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha VETA mjini Singida.Kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Singida, Mohammed Likwata akitoa taarifa yake kwenye mkutano wa madereva wa magari ya abiria ulioitishwa na SUMATRA.
Baadhi ya madereva wa magari ya abiria waliohudhuria mkutano ulioitishwa kwa ajili yao na SUMATRA.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Madereva nchini wamehimizwa kuanzisha vyama vyao ili kujijengea mazingira mazuri ya kuweza kukabiliana kisayansi na changamoto zinazowakabili ikiwemo ya kulipwa maslahi duni na waajiri wao.
Wito huo umetolewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa SUMATRA,Ahmad Kilima wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa madereva wa magari ya abiria mkoani Singida.
Alitaja changamoto zingine zinazowakabili madereva,kuwa ni kutokuwa na ajira za uhakika na uwezo mdogo wa kujisomesha au kujiendelea kielimu,ili kuwa na ufahamu mkubwa wa sheria na kanuni za usalama barabarani.
Kaimu meneja huyo alisema SUMATRA inaamini kuwa wamiliki wa mabasi na malori au waendeshaji wa makampuni ya mabasi na malori na madereva wenyewe,kwa pamoja wanayo nafasi kubwa ya kuchangia kupunguza ajali nchini.