Makamu wa Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) Bw. Phares Magesa.
1. Kombe la Taifa (Taifa
Cup 2012) kufanyika Tanga
Nachukua fursa hii
kukutaarifu kuwa mashindano ya kombe la Taifa (Taifa Cup) mwaka huu yatafanyika
Tanga tarehe 29 /10/2012 hadi 4/11, 2012.
Mashindano haya ya Kombe la
Taifa kwa kawaida ndio hutumika kuchagua timu zetu za Taifa, hvyo ni muhimu kwa
mikoa yote kushiriki ili kuwapa nafasi wanamichezo kutoka mikoa yao kuonekana
katika ngazi ya Taifa.
Mikoa iliyothibitisha hadi
sasa ni Iringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Singida, Mara, Dodoma,
Pemba, Unguja, Tanga, Mtwara, Lindi na Dar Es Salaam.
Bado nafasi ya kuthibitisha
kushiriki ipo kwa wanaopenda kushiriki katika mashindano haya na ratiba ya
mashindano itapangwa tarehe 28/10/2012 katika kikao ambacho wawakilishi wa mikoa
yote lazima wawepo na ndo itakuwa mwisho wa kuthibitisha
kushiriki.
2. Walimu wa Taifa wa Mpira
wa Kikapu toka Marekani:
Awali tulitangaza kuhusu
ujio wa Makocha wa kikapu toka Marekani kuja kufundisha timu yetu ya Taifa,
ambao ni Albert Sokaitis (Kocha Mkuu) ambaye ni Kocha mwenye uzoefu wa miaka 24
kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya Chuo Kikuu cha Post huko huko Marekani katika
jimbo la Connecticut. Pia amewahi kufundisha timu na kuendesha mafunzo nchi za
Uchina, Lebanon, Ugiriki na Japan.
Ambaye atasaidiwa na Kocha
Jocquis L. Sconiers ambaye nae ana uzoefu wa miaka mingi na kwa sasa ni Kocha
Mkuu Msaidizi wa timu ya Chuo Kikuu cha Post huko Marekani katika jimbo la
Connecticut.
Walimu wote hawa wana
shahada za juu kutoka vyuo vikuu mbali mbali vya
Marekani.
Katika utekelezaji wa
mpango huo katika awamu ya kwanza Kocha Sconiers anatarajiwa kuwasili nchini
tarehe 30/10/2012 na ataelekea Tanga siku inayofuata katika Mashindano ya Kombe
la Taifa ili kuchagua wachezaji watakaonda timu za Taifa (wanawake na wanaume)
na baada ya hapo ataanza mafunzo rasmi kwa timu zote 2 tarehe
5/11/2012.
Awamu hii ya kwanza ya
mpango wa mafunzo unadhaminiwa na watu wa Marekani kupitia ubalozi wao hapa
Tanzania, tunawashukuru sana watu wa Marekani.
3. Mashindano ya Kanda ya
tano ya FIBA Afrika
Kama mipango yote ikienda
vizuri tunatarajia Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano ya kanda ya 5 ya
FIBA. Mashindano haya yanayotarajiwa kufanyika hapa Dar Es Salaam kuanzia 15
hadi 22 Desemba, 2012.
Hivyo basi Kocha huyo
atatumia nafasi hii kuanza maandalizi ya timu zetu za Taifa kuziandaa kwa
mashindano haya yanayotarajiwa kushirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Misri Sudan na Sudani ya
kusini.
4. Mkutano Mkuu wa
TBF
Tunatarajia pia kufanya
Mkutano mkuu wa TBF na wa bodi kwa mujibu wa katiba siku ya tarehe 1 hadi 2
Novemba, 2012. Viongozi wote wa Mikoa na wawakilishi wachezaji, vyama shiriki
wanaombwa kushiriki bila kukosa katika mkutano huu utakaofanyika
Tanga.
Tunaomba wadau wote mtuunge
mkono kwa hali na mali kufanikisha malengo yetu ya muda mfupi, wa kati na muda
mrefu kwa faida ya vijana wetu na Taifa letu.
Mungu Ibariki
Tanzania
PHARES
MAGESA
MAKAMU WA
RAIS-TBF
Post a Comment