Meneja mradi wa shirika lisilo la
kiserikali linalowajengea uwezo wajasiriamali kwa kutumia teknolojia ya habari
na mawasiliano katika kupambana na umaskini( EIFL) Monica Elbert (mzungu)
akipokea maelezo kwa mjasirimali Geofrey Nkong’o (wa pili kushoto) huko Kitunda
-DSM kuhusu watakavyonufaika na mafunzo waliyoyapata kupitia
mpango wa kufundishia wa teknolojia ya habari na mawasiliano ujulikanao (Public
Library Innovation Programme- PIP) ambapo, shirika hili linafadhili Maktaba ya
Taifa nchini (TLSB) ili ziweze kutumia teknolojia hiyo katika kuwaletea
mawasiliano wajasirimali katika kupata habari kwa ajili ya matumizi mbalimbali
katika shughuli zao za kila siku na maendeleo.
Meneja
mradi wa shirika la (EIFL) Monica Elbert kutoka Ujerumani (kulia)
akimsikiliza Katibu wa kikundi cha wajasiriamali wa Kiyombo Kitunda mkoani Dar
es Salaam Yesaya Mbwambo, (katikati) wakati wakiangalia baadhi ya mabanda ya
ufugaji wa kuku na jinsi wajasiriamali watakavyonufaika
baada ya kumaliza mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasliliano,
ambapo wataweza kutafuta taarifa mbalimbali kupitia mtandao na
zikiwepo za utafutaji wa masoko pamoja na shughuli zao za kila siku, (kushoto)
ni Mwenyekiti wa kikundi cha (KUK) Wambura Mugasa.
Meneja mradi washirika lisilo la kiserikali kutoka Ujerumani (EIFL)
Bibi Monica Elbert (kulia) akiwashukuru wanakikundi wajasiriamali cha ufugaji
kuku wa Kiyombo Kitunda (KUK) baada ya kumpatia zawadi ya vazi la
kitenge kwaajili ya kumbukumbu, baada ya kuwatembelea mishoni mwa wiki na
kuangalia shughuli zao za ufugaji. Picha na Mwanakombo Jumaa-
MAELEZO
Post a Comment