Hapa baadhi ya waislamu walioamua liwalo naliwe na kuamua kuwatunishia msuli polisi na kusema pigeni mpendavyo hatoki mtu.
|
Askari
wa jeshi la Polisi kikosi cha kutuliza ghasia wakiwadhibiti vijana
waliokuwa wakileta vurugu eneo la mbagala kufuatia kijana mmoja
anaesemekana anasoma kidato cha kwanza kukojolea mkojo Quraan na
kusababisha hasira kwa waisilamu hassa vijana ambao walitapakaa mitaani
na kuanza kuleta vuru. |
|
Vijana waliosambaa mitaani na kuamsha vurugu kubwa kwenye eneo hilo la Mbagala Kizuiani.
|
Hili ni moja kati ya makanisa
matatu yaliyovunjwa, hapa baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia vioo
vilivyovunjwa kwenye Kanisa hilo Jipya la Wasabato lililopo upande wa
magharibi mwa karibu na kituo cha mabasi kizuiani. |
|
Barabara zilifungwa kwa mawe na askari kupata wakati mgumu kupita. |
|
Barabara zilizuiwa na matariri yaliyochomwa moto |
|
|
Waisilamu
waliotoka msikitini kwenye swala ya Ijumaa walikumbana na kimbembe cha
kamatakamata hatakama hawakuwemo kwenye sakata hilo, alama ni kanzu na
sijda |
|
Barabara zilikua zikiharibiwa kwa moto ulikuwa ukiwashwa na waisilamu hao wenye hasira. |
|
Maji ya kuwasha yalikuwepo ingawa hayakuweza kuzuia vurugu hizo. |
|
Askari na watuhumiwa wakivuka pamoja kwenye mtaro wa maji taka. |
|
Watuhumiwa wavurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi. Picha na Mtaa kwa Mtaa Blog |
on Saturday, October 13, 2012
Post a Comment