Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TRAWU WATAKA TAZARA IGAWANYWE

 
CHAMA cha Wafanyakazi wa Reli nchini (TRAWU), kimetishia kugoma iwapo Serikali haitatekeleza madai yao ya kuligawa Shirika la Reli la Tanzani na Zambia (TAZARA), ili kila nchi ijiendeshe yenyewe.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Erasto Kihwele, alisema uwamuzi huo umefikiwa hivi karibuni kwenye mkutano wa kujadili kwa kina hali ya uendeshaji wa shughuli za Reli nchini, uliyofanyika mjini Morogoro.
Alisema wamefikia hatua hiyo kutokana uendeshaji shirika hilo kuwa mgumu sana kutokana na maamuzi mengi kuingiliana katika utekelezaji wake.
“Tunataka tugawane reli kiuendeshaji, Tanzania kivyake na Zambia kivyake vinginevyo uendeshaji utasimama toka Dar es Salaam hadi Tunduma”alisema Kihwele.
Aidha, wafanyakazi wote wanaanza vikao kuanzia kesho, katika kanda za Dar es Salaam, Mlimba na Mbeya kwa ajili ya kujadili hoja nzito kama vile kukosekana mafuta tangu Oktoba 21 mwaka huu ya magari moshi ya mizigo ambapo iiliwafaya wafanyakazi kurudishwa nyumbani.
Hoja nyingine ni kurudishwa kwa mameneja saba waliokuwa wamesimamishwa kazi, muundo wa mshahara, posho za kazi katika mazingira magumu, ucheleweshwaji wa mishahara.
Vilevile malimbikizo ya makato ya wafanyakazi ya mifuko ya Hifadhi ya jamii, ilipwe kuanzia mwezi Septemba mwaka huu ya jumla ya milioni 258 ili waanze kupata mafao wanayostahili kuanzia mwezi huo.
Akizungumzia kuhusu Shirika la Reli Tanzania (TRL), Kihwele alisema wanamtaka Waziri Mkuu awapatie fursa ya kzungumza naye kuhusu utata wa serikali kumiliki shirika hilo kwa asilimia 100.
Ili kumaliza utata kuhusu nyaraka na zinazoonyesha kuwa kweli serikali imevunja mkataba uliyokuwepo hapo awali na wawekezaji kutoka nchini India.
Alisema maombi yao kwa serikali, itoe tamko kwa maandishi kuhusu kumiliki Reli hiyo kwa asilimia 100 kutokana na kuwa hilo ndio hitaji kubwa kwa taasisi za fedha (NBC).
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top