Fabrice Muamba akiwa na furaha tele baada
ya kukaribishwa kwa shangwe na shauku na wadau.
Kutoka Kulia CEO wa Beffta, Pauline Long
akitaja washindi wa tuzo za mwaka 2012.
Mtangazaji Nguli wa zamani wa ITV sir
Trevor McDonald akisema machache baada ya kupokea Tuzo ya Beffta ''LIFE TIME
ACHIEVEMENT ''.
Makamuzi
yakiendelea.
Frank
Eyembe akila pozi na Fabrice Muamba.
Frank
akiwa na Actor Wale Ojo baada ya kunyakua tuzo ya best actorkutoka kulia Mshindi
wa best of Best Fashion Choreographer 2012 Yvonne, Jestina, Peace na
Frank.
kutoka kulia Mshindi wa best of Best
Fashion Choreographer 2012 Yvonne, Jestina, Peace na
Frank.
sehemu ya kadamnasi ilivyofurika wadau
kutoka sehemu mbalimbali.
Warembo waking'ara ndani ya red
Carpet.
Catwalk Professor akila pozi baada ya
kushinda tuzo yake ya Beffta.
Urban Pulse na Miss
Jestina blog wanakuleta taswira mbalimbali kutoka katika tuzo za Nne Beffta 2012
zilizofanyika Jumamosi tarehe 27 Oktoba 2012 ndani ya Ukumbi wa HIPPODROME,
GOLDERS GREEN, LONDON NW1 7RP. Tuzo hizi ziliandaliwa maalum kwa ajili ya
kutambua michango mbalimbali ya wasanii na wataalam katika tasnia ya Luninga,
Filamu, Internet, Mitindo, Magazeti, Majarida, Muziki,Tamthilia,Tovuti na Blogs,
Kucheza, Mashairi, na michango ya watu fulani mashuhuri katika kukuza au
kuimarisha jamii ya watu weusi hususani Wafrika waishio hapa nchini
Uingereza.
Mojawapo ya tuzo za muhimu
Beffta zilikwenda kwa mtangazaji nguli wa zamani wa ITV, Sir Trevor Mcdonald
aliejinyakulia tuzo ya "Life time Achievement" kutokana na mchango wake katika
tasnia ya utangazaji.Mbali na hapo tuzo za Beffta zilienda maili zaidi kwa kumkaribisha mchezaji wa zamani kutoka timu ya Bolton ambaye alifariki uwanjani kwa muda wa dakika 54, lakini kutokana na nguvu pamoja na miujiza ya Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha madaktari aliweza kufufuka na kuwa hai hadi leo hii. Mchezaji huyu mwenye asili ya Kikongo aitwaye Fabrice Muamba alifunga pingu za maisha hivi karibuni na mchumba wake Shauna Magunda pia ndio aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizi za tuzo za Beffta 2012.
Tuzo za Beffta zimeanzishwa miaka minne iliyopita na Pauline Long kutoka Kenya ambaye ndiye CEO wa tuzo za Beffta.
Asanteni,
Urban Pulse wakishirikiana na Miss Jestina Blog
Post a Comment