Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANANCHI WALILIA MIPAKA YA MBUGA YA SAADANI


WANANCHI wa Kijiji cha Kitame Tarafa ya Mwambao Wilaya ya Bagamoyo, wameiomba Serikali kuainisha mipaka kwa haraka ili kupunguza migogoro iliyopo kati yao na Hifadhi ya Wanyamapori ya Sadani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi mwishoni mwa wiki Mwenyekiti wa Kijiji cha Kitame, Sylivester Kangwe alisema kumekuwepo na mgogoro wa muda mrefu wa mipaka kati ya kijiji hicho na TANAPA lakini licha ya kuwa na malalamiko mengi toka kwa wananchi Serikali bado inasuasua kumaliza tatizo hilo.
Kangwe alisema mgogoro wa mipaka katika eneo lake umekuwa sugu hali inayopelekea wananchi wake kupata adha nyingi, ikiwemo ya kutakiwa kulipa kiasi cha Sh.1000 kufika kijiji cha jirani ambacho nacho hakipo katika eneo la hifadhi.
Aidha wameitaka TANAPA kuondoa kizuizi hicho katika ardhi ya wananchi na kukipeleka katika eneo lao la hifadhi ili wananchi wawe huru kutembeleana na kupata huduma muhimu katika jamii yao kwani vijiji hivyo vilivyowekewa kizuizi vinategemeana.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi amekiri kupata malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na kudai kuwa yanashughurikiwa kwa mujibu wa taratibu na sheria na hatimaye yatatolewa majibu.
Hata hivyo Kipozi akiwa katika ziara ya ghafla katika eneo kilipo kizuizi hicho alishuhudia wananchi waliolipishwa huku wakiwa na risiti zao za kupita katika kizuizi hicho, hali iliyompelekea kuwataka askari wa TANAPA kusitisha kuwalipisha wananchi.
Aidha aliwataka askari hao kuacha kuwanyanyasa wananchi kwa namana yoyote ambapo aliwapa namba yake ya simu viongozi wa vijiji vinavyotumia kupita katika kizuizi hicho kilichopo katika daraja la mto wami ili waweze kumpa taarifa endapo wananyanyaswa na askari hao.
Hata hivyo, Kipozi aliahidi kufanya mazungumzo ya haraka na Mkuu wa Hifadhi ya Sadani ili kuweka njia ya sahihi ya kutekeleza majukumu yao.
Naye Afisa Mipango Miji wa Wilaya ya Bagamoyo, Clemence Mkusa alisema suala la mipaka katika vijiji hivyo tayari limeshashughurikiwa na mapendekezo yake yapo Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top