Kwa wiki nzima nimekuwa nakusanya
mawazo, kutoka kwa wapenzi mbali mbali ambao walikuwa wananisaidia uchunguzi
wangu juu ya namna wanavyoshiriki tendo la ndoa na
kulidhika.
Wengi kati ya hao kwa kiwango tofauti
cha kuanzia mara tatu na kuendelea waliniambia kuwa hawatosheki na viwango hivyo
na kuliacha swali kubaki kuwa wapenzi wakutane mara ngapi kwa wiki ili
watosheke?
Jibu la swali hili linapatikana baada
ya kutambua kitu kimoja muhimu, nacho ni chanzo cha kutosheka hasa nini? Katika
hali ya kawaida kutosheka kupo zaidi akilini na wala si mwilini, hii ina maana
kwamba watu wanaodhani kuupa mwili mahitaji zaidi kadiri unavyodai ni njia ya
kuutosheleza wanajidanganya, kwa sababu tamaa ya mwili haitoki mwilini bali
kwenye akili ya mtu.
Kwa msingi huo mtu akitaka kutosheka
na penzi la mpenzi wake, ni lazima kwanza aitosheleze akili yake na kile
anachopata, zoezi ambalo atalifikia kwa kutathimini uwezo wake wa kufanya
mapenzi na wa mpenzi wake. Wengi kati ya watu wanaodai hawatosheki kimapenzi ni
wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo,
nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.
Nikijibu swali la ni mara ngapi
wapenzi wakutane kimwili ili watosheke nitasema hivi: KUTOSHEKA HAKUNA IDADI,
bali ni kwa kila mmoja kulidhika na mwenza wake kutoka ndani ya akili yake. Kama
hapa sikueleweka vizuri katika jibu hilo, maana yangu hasa ni kwamba kutosheka
ni namna mtu mwenyewe anavyoyaendesha mawazo yake.
Ukiyaendesha mawazo yako kufanya
mapenzi mara kwa mara, hutatosheka hata ukipewa kila saa, kwa sababu fikra zako
unazijenga zaidi ya unachopata. Uchunguzi unaonesha kuwa watu ambao akili zao
zimejaa mawazo ya ngono, hawawezi kulala bila kufanya mapenzi, lakini watu hao
hao, ukiwapa matatizo yatakayochukua sehemu kubwa ya mawazo yao kwa mfano,
kuwafunga jela, kuwafukuza kazi, kupata msiba, utashangaa wanaweza kukata wiki
bila kusumbuliwa na tamaa ya ngono.
Hii ina maana kwamba unavyowaza ndivyo
unavyotenda. Kitaalamu kinachofanya mapenzi ni mawazo, ndiyo maana wapo
wanaojichua wenyewe kwa kutumia mawazo yao na kupata raha. Kila mmoja akijenga
heshima juu ya fikra zake na kujali hisia zaidi tutakuwa na watu wengi
wanaofurahia tendo la ndoa bila kujali wanalipata mara ngapi kwa
wiki.
Uchunguzi wangu umebaini kuwa watu
wengi hasa wapenzi wa siku nyingi na wanandoa, wanafanya mapenzi kwa sababu tu
wamepata nafasi ya kuwa pamoja, lakini si kwa kuheshimu fikra na hisia zao,
jambo ambalo husababisha ladha ya mapenzi kuwa ya asilimia ndogo, ukilinganisha
na mahitaji halisi ya mawazo yao.
Upo ushahidi wa kutosha kwa wanandoa
wengi kupata msisimko mdogo wanapokuwa na waume/wake zao katika tendo la ndoa
tofauti na wanapopata wasaa wa kusaliti ndoa kwa hawara zao.
Watu wa aina hii wasiseme kuwa
hawatosheki na tendo la ndoa kwa sababu wanakutana na wapenzi wao mara chache
zaidi, bali wanakutana katika mhemko wa chini usioweza kulifanya tendo hilo kuwa
na raha ya kutosha.
Labda msomaji wangu utaniuliza, tatizo
la kupata msisimko mdogo kwa mtu unayemzoea linachangiwa na nini? Jibu litakuwa
ni MAWAZO ya mtu mwenyewe.
Ukichunguza utagundua kuwa, wapenzi
wengi hasa wazoefu huwa hawapeani nafasi katika mawazo, kama wanavyotoa nafasi
kwa wapenzi wa pembeni, hili ndilo tatizo linalopunguza msisimko wa kimapenzi na
kuondoa hali ya kutosheka na penzi. Kama mtu anataka mpenzi wake amtosheleze,
basi hana budi kumkuzia mwenza wake hisia kiasi cha kumtamani. Niulize swali,
hivi ni mara ngapi wewe unayesema hutosheki na penzi ulishakaa
peke yako ukamvutia taswira mpenzi wao kabla hajarudi nyumbani
kiasi cha kupata msisimko wa kutana naye kimwili?
Wengi wetu hatufanyi hivyo, hatuna vitu
vinavyotuvutia kwa wake/waume zetu, jambo ambalo hutufanya tukikutana nao
kimwili kwa kutimiza desturi tu na kubaki na kiu zetu za penzi. Lakini uweli
unabaki kuwa wapenzi wakikutana kipindi cha msisimko mkubwa na kupeana mahaba
kwa usahihi hata ikiwa ni mara moja kwa wiki watatosheka.
Jambo kubwa
la kuzingatia hapa ni kwamba wakati mwingine msisimko huo huwa hauwatokei
wapenzi kwa wakati mmoja, hivyo ni jukumu lao kushirikiana pindi
mmoja anapokuwa katika hali hiyo.
CHANZO: UjanaTz
Post a Comment