Mshiriki wa shindano la Redd's Miss
Tanzania 2012, Mary Chizi akicheza mchezo wa pool dhidi ya Timu ya TBL Arusha.
Warembo hao jana walitembelea kiwanda hicho cha Bia cha TBL mjini Arusha wakati
walipofanya ziara maalum. Warembo hao wapo Mikoa ya Kanda ya Kaskazini
kutembelea Vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Afisa Usalama mahali pa kazi wa Kampuni
ya Bia Tanzania Tawi la TBL Arusha, Heavy Kasena akiwapa maelezo ya shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Kiwanda hicho cha TBL mjini Arusha warembo wa
wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 walipotembelea kiwanda hicho jana.
Washiriki wa shindano la Redd's Miss
Tanzania 2012 wakipita katika maeneo mbalimbali ya kiwanda cha Bia cha TBL
mjini Arusha wakati walipofanya ziara maalum. Warembo hao wapo Mikoa ya Kanda
ya Kaskazini kutembelea Vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani
nchini.
Washiriki wa shindano la Redd's Miss
Tanzania 2012, wakicheza mziki aina ya Kwaito mara baada ya kumaliza ziara yao
ya kutembelea Kiwabnda cha TBL cha mjini Arusha jana. Warembo hao wapo Mikoa ya
Kanda ya Kaskazini kutembelea Vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani
nchini
Post a Comment