Na
Mwandishi Wetu
WAKATI
zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Redd’s Miss Tanzania 2012 kupatikana,
imezuka hofu kubwa ndani ya kambi ya warembo hao 30 wanaowania taji hilo, huku
kila mshiriki akibaki na swali lisilo na jibu kichwani mwake kuwa nani atatwaa
taji hilo.
Redd’s
Miss
Tanzania
2012, atajitwalia gari pamoja na fedha taslimu Sh. milioni 8, katika
kinyang’anyiro hicho kinachotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue
Pearl uliopo jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam siku ya
Jumamosi.
Wakizungumza
na mtandao huu, kwa nyakati tofauti katika kambi ya timu hiyo iliyopo hoteli ya
Giraffe, Dar es Salaam warembo mbalimbali walisema washiriki wote kwa sasa wana
hofu tupu.
“Pamoja
na kuingia 15 bora ya Redd’s Miss Tanzania mpaka sasa, lakini bado sina uhakika
kama nitatwaa taji, maana kila mrembo namuona yuko bomba na kujiamini kuliko
hata mimi” alisema Redd’s Miss Photogenic, Lucy
Stephano.
Mpaka
sasa washiriki watatu waliofanikiwa kuingia hatua ya 15 bora ni Lucy pamoja na
Mary Chizi aliyetwaa taji la Miss Sports Lady na Babylove Kalala aliyefanikiwa
kushinda lile la Redd’s Miss Talent.
Warembo
hao wawili pia walizungumzia ugumu wa shindano hilo, huku Mary akisema kuna kazi
kubwa na Babylove akidai kila kitu kwa sasa amekiacha mikononi mwa
Mungu.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga, ambao ndio waandaaji wa shindano
hilo alisema, kila kitu kwa sasa kimekamilika na wana imani kubwa shindano
litakuwa kali na la kuvutia.
“Tumekamilisha
kila kitu, naamini atapatikana mrembo mkali zaidi ambaye atatuwakilisha vema
katika mashindano ya dunia,” alisema.
Naye
Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original walio wadhamini wakuu wa shindano hilo,
Victoria Kimaro, alisema huu ni wakati sahihi wa kumpata mshindi bomba mwenye
vigezo.
“Kwa
jinsi mambo yalivyo, nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya shindano,
maana hili litakuwa ni shindano la kipekee,”
alisema.
Shindano
hili la Redds Miss Tanzania 2012 linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia kinywaji cha Redds Original.
Post a Comment