Umoja wa Watanzania mjini Wuhan, China
(WUTASA) jana ulimchagua kuwa Mwenyekiti wake kwa kipindi cha mwaka
mmoha ujao 20012/20013).
Dr. Gululi anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Bi Fatma Waziri aliyemaliza muda wake wa uongozi kwa
mujibu wa Katiba ya umoja huo. Aidha Bwana Hamphrey Skauki ameendelea
kuitetea nafasi yake ya Ukatibu wa WUTASA kwa kipindi kingine cha mwaka
mmoja. Simon Kahwa alichaguliwa kuwa Mweka hazina nafasi ambayo awali
ilikuw aikishikiliwa na Bi Felister Mahuya aliyemaliza muda wake
Uchaguzi huo umefanyika kwa
mujibu wa vifungu 5.2.1 na 6.1 vya katiba ya WUTASA vinavyoelekeza jinsi
ya kuwapata viongozi wa WUTASA na muda wao wa kukaa madarakani kwa
vipindi visivyozidi viwili vya mwaka mmoja mmoja.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa,
Dr. Gululi aliwaomba Watanzania mjini Wuhan kuwa kitu kimoja na
kutangaza sifa nzuri za Tanzania.
“Katika muda wote tutakao
kuwa hapa mjini Wuhan, tunatakiwa kuweka uzalendo mbele, kwa
kushirikiana katika mambo mbalimbali yanayotakiwa kutekelezwa kwa mujibu
wa mpango kazi wa umoja wetu,” alisema.
Aidha alieleza kuwa katika k
ipindi chake cha uongozi atahakikisha anabuni vyanzo vingine vya mapato
kwa kushirikiana na wanaWUTASA badala ya kuendelea kutegemea ada za
wanachama pekee.
awali akisoma taarifa ya mwaka wa
uongozi uliopita Bwana Skauki aliwaeleza wajumbe wa mkutano mkuu kuwa
uongozi ulifanikiwa kuitangaza Tanzania vema katika maonesho ya
utamaduni ambayo kila mwaka hufanyika katika chuo kikuu cha WUHAN.
“Kwa mwaka 20011/2012, uongozi
kwa kushirikiana na kamati ya Social, tuliweza kuitangaza nchi yetu
Tanzania katika maonesho ya Utamaduni yanayofanyika kila mwaka chuoni
Wuhan,” alisema. Maonesho ya mwaka jana yalishikisha watu kutoka zaidi
ya mataifa 70 duniani.
Aliongeza kuwa fursa hii
imewafanya watu wa mataifa mbalimbali ambao awali hawakujua vivutio
vinavyopatikana Tanzania ukiwemo utamaduni wa wananchi wake kuuijua na
kuendelea kutaka kupata taarifa za mambo mbalimbali yanayohusu Tanzania.
Post a Comment