Wiki hii imeanza na zali zaidi ya lile la mentali kwa
mtoto ambae alikuwa anaishi katika mazingira magumu sana nchini Kenya, inaweza
kuwa ndoto alizoota zikmekuwa kweli na kama hakuwahi kuota basi Mungu
amemsapraiz na kujikuta anapata deal la uhakika la kufanya muziki chini ya lebel
kubwa duniani ya ‘Konvict’.
Mtoto huyo anaeitwa Wilson alimsimamisha Akon wakati
anaelekea kupiga show pande hizo na akaona kabisa kuwa hii ilikuwa ni chance ya
yeye kumueleza Akon ya moyoni tena sio kumuomba mkwanja ila ni kumuomba kujiunga
na lebel ya Konvict. Duh, unaweza kudhani mtoto huyo alikuwa mwehu eeeh…dogo
alirusha mkuki vizuri!!
Baada ya Akon kukubali kusimama tu mtoto huyo
alizitumia dakika chache kumsimulia hali mbaya ya maisha anayoishi na jinsi
ambavyo baba yake alivyomtesa na kulazimika kulala nje, akaeleza jinsi gani
anavyoupenda muziki na hana jinsi ya kuweza kuingia studio kurekodi.
Surprisingly, Akon akaamua kumpa nafasi, akaingia nae kwenye gari lake na
wakaelekea wote kwenye concert yake.
Hatujui nini kiliendelea kwenye gari lakini inaonekana
waliendelea kuongea kuhusu yale waliyoyaanzisha. Na haikuwa raisi kwa Akon kumpa
nafasi kirahisirahisi tu.
Wakati anaendelea na performance yake mkali huyo toka
Senegal alimuita stejini yule mtoto. Kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa kubwa na
Akon, dah, hii ni bahati ama baraka?! Akon akamkabidhi dogo mic na kumwambia
aperform!
Ni kama ulikuwa mtihani wa mwisho kwa dogo huyo ambao
ungemtoa lawama Akon kirahisi, dogo alifunika vibaya na kuonesha kipaji kikubwa
alichonacho.
Haikuhitaji press release ama press conference
kutangaza uamuzi wa Akon, alishika mic na kutangaza mbele ya umati wa watu,
“Wilson the newest member of the Konvict family”. Ni hivyo tu dogo anachukua
pipa kwenda kuishi ndoto zake Marekani.
Huyu ni mtoto wa kiafrika mwenye story ya mafanikio
inayofanana na ya Akon.
Post a Comment