Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ANAYETUHUMIWA KUMUUA DAUDI MWANGOSI LEO KUPANDISHWA MAHAKAMANI TENA


MTUHUMIWA wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi (Leo) atafikishwa tena mbele ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.

Mtuhumiwa huyo askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa ambaye alipashwa kufikishwa mahakamani hjapo Novemba 14 mwaka na kutofikishwa kwa madai ya gari la mahabusu kukosa mafuta , huku wananchi wengi wakijitokeza kushuhudia mtuhumiwa huyo bila mafanikio leo wamejipanga kufika tena mahakamani hapo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Iringa walisema kuwa wataendelea kufika mahakamani hapo hadi kesi hiyo itakapofika mwisho.

Huku kwa upande wao wanahabari mkoa wa Iringa wakidai kuwa wapo tayari kuendelea kusitisha shughuli zao nyingine ili kufuatilia suala hilo zaidi. Katibu mtendaji wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard aliwataka wanahabari mkoa wa Iringa kuendelea kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo .

Hata hivyo wanahabari hao wamehoji sababu ya jeshi la polisi kumfikisha mtuhumiwa huyo huku akiwa amefunikwa uso wake tofauti na watuhumiwa wengine.

Mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top