Waziri wa Maliasili na Utalii Mh . Balozi Khamis Kagasheki akikabidhi zawadi ya Kinyago Leila Ansell kutoka kampuni ya Zara Tours Adventures mara baada ya kuwa miongoni mwa makampuni ya utalii Tanzania yaliyopewa tuzo kwa ajili ya kuuza na kutangaza utalii wa Tanzania vizuri katika maeneo mbalimbali duniani hasa Marekani na Ulaya katika Dhifa iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) kwa makampuni yanayoshiriki maonyesho ya Utalii ya Dunia World Travel Market (WTM)katika eneo la Excel jijini London nchini Uingereza , ambapo Balozi Khamis Kagasheki alikuwa mgeni rasmi katika dhifa hiyo akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe.
Katika picha katikati
anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)Bw.
Geofrey Meena
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh . Balozi Khamis Kagasheki akikabidhi tiketi ya ndege
kwa Bw. Kamuhanda tiketi iliyotolewa na shirika la ndege la Precision Air
nchini Tanzania ambao nao wameshiriki katika maonyesho hayo ya utalii ya WTM
nchini Uingereza, Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa shirika hilo Bw. Patrick
Ndekana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh . Balozi Khamis Kagasheki akikabidhi tuzo kwa Bw. John
Bukuku Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mtandao wa www.fullshangweblog.com kutokana na
mchango wa mtandao huo katika kutangaza utalii nchini Tanzania na duniani kote
katikati ni Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) Bw Geofrey
Meena.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh . Balozi Khamis
Kagasheki akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Pongo Safari & Tours Bi. Cynthia
Ponera katika hafla ya kutambua na kupongeza mchango wa makampuni mbalimbali na
kuwazawadia kutokana na kazi nzuri ya kuuza na kuutangaza utalii wa Tanzania,
katikati ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey
Meena.
Bw.
Hans Warburg Mkurugenzi wa Masoko wa Pongo Safari & Tours akipiga picha ya
pamoja na Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki mara baada ya kampuni yao
kujinyakulia tuzo hiyo.
Mwanahabari Angela Msangi kutoka Shirika la
Utangazaji la Taifa TBC akiwajibika vilivyo katika maonyesho ya WTM nchini
Uingereza kama anavyoonekana katika picha akiwa ameshika video Camera akiendelea
na majukumu yake..
Waziri wa
Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika dhifa hiyo kabla
ya kukabidhi tuzo kwa makampuni yaliyofanya vizuri katika kuuza na kutangaza
utalii wa Tanzania, wa pili kutoka kulia ni Balozi Peter Kallaghe watatu kutoka
kulia ni Issa Ahmed Othman Mshauri wa Rais Zanzibar Masuala ya Utalii na kulia
ni Bw Yusuf Kashangwa Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara Ubalozi wa Tanzania
nchini Uingereza.
Mkurugenzi wa
Biashara Shirika la ndege la Precision Air nchini Tanzania Bw. Patrick Ndekana
akiwa na Yvonne Baldwin kutoka shirika hilo wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea
katika dhifa hiyo iliyofanyika kwenye banda la Tanzania.
Rais
wa Kampuni ya Bradford Group kutoka nchini Marekani BiKarren Hoffman ambaye ni
mwakilishi wa bodi ya Utalii (TTB)nchini Marekani akiongea katika hafla hiyo ,
ambapo ameyapongeza mashirika mbalimbali yanayofanya kazi kwa karibu na na Bodi
ya Utalii Tanzania kwa jinsi yalivyosaidia kukuza utalii wa Tanzania , katikati
ni Mkurugenzi wa Masoko wa (TTB) Devotha Mdachi na kushoto ni Meneja Masoko wa
(TTB) Bw. Geofrey Meena
Post a Comment