Mbunge wa Kigoma Kaskazini
Zitto Kabwe akichangia kwa hisia katika semina ya wabunge juu ya fao la kujitoa,
kwenye ofisi za bunge mjini Dodoma leo.
Wabunge wa bunge la
Tanzania wamegawanyika katika semina yao juu ya fao la kujitoa katika mifuko
ya hifadhi ya jamii ambapo wabunge wengi vijana wanataka mifuko hiyo irudishe
sheria ya kujitoa wakati mawaziri na baadhi ya wabunge wengine wanakataa
kurudishwa kwa fao hilo.
Kuna hoja zingine za
wabunge zinazotaka sheria ya fao la kujitoa lisiwepo na badala yake kuwepo fao
lingine la kujikimu kwa wanachama wanaoachishwa kazi wakati wakisubiri umri wao
wa kupata fao la kujitioa.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini
Zito Kabwe (Chadema) amesema kuwa kwa sasa fedha nyingi za mifuko ya hifadhi
ya jamii zinatumika vibaya kwa kisingizio cha uwekezaji na masuala mengine
yanayofanana na hayo na kusababisha hofu kubwa ya uwezo wa mifuko hiyo
kuwalipa wanachama wake hapo baadaye.
Amesema kuwa yeye hatakuwa
tayari kuona kuwa mifuko hiyo haina fedha ya kuwalipa wanachama wanaofikisha
umri wa kupata fao la kujitoa, endapo kama atakuwa Rais wa nchi yetu ya
Tanzania .
Zito amesema kuwa hata
kama siye yeye atakuwa Rais wa Tanzania miaka ijayo, laikini hatapenda kuona
mtu yeyote atakayekuwa Rais akishindwa kuwalipa mafao wanachama wa mifuko
hiyo.
Usemi wa Zitto ulileta
minong’ono kutoka kwa wabunge na Spika aliyekuwa anahudhuria semina hiyo katika
ukumbi wa zamani wa Bunge kwa sasa unaitwa ukumbi wa Pius
Msekwa.
Post a Comment