MWANAMUZIKI Mary Jane Blige ni kati ya
wanamuziki mahiri wa Marekani.Blige, aliyezaliwa Januari 11, 1971, pia anasifika
kutokana na kuwa prodyuza na kucheza filamu.
Ameshinda tuzo tisa za Grammy na American
Music Award kutokana na muziki wa R&B, Rap, Gospel na Pop.
Blige alianza muziki mwaka 1992 baada ya kutoa
albamu ya kwanza aliyoipa jina la 'What's the 411'.
Mwanamuziki huyo ameuza zaidi ya nakala
milioni 50 za albamu za muziki sehemu mbalimbali duniani.
Anahesabiwa kuwa miongoni mwa wanamuziki wa
R&B wenye mafanikio zaidi katika kipindi cha miaka 25.
Blige pia amejizolea sifa kubwa kutokana na
kazi zake za filamu na manukato.
Aling'ara katika filamu ya Tyler Perry
iliyotolewa mwaka 2009.
Mwanamuziki huyo anakadiriwa kuwa na utajiri
wa kiasi cha Dola 45 milioni (Sh 70 bilioni).
Mwaka 2004, alianzisha lebo ya Matriarch
Records na amekuwa akisambaza kazi za wanamuziki mbalimbali.
Pia anatengeneza manukato yanayoitwa My Life
na My Life Blossom HSN.
Blige pia ana kampuni ya kutengeneza miwani ya
jua ya "Melodies by MJB".
Pia anafanya shughuli za matangazo na kampuni
za Reebok, Air Jordan, Pepsi, Coca-Cola, Gap, Target, American Express, AT&T
Inc., M∑A∑C, Apple Inc., Burger King na Chevrolet.
Mwanamuziki huyo anaishi Saddle River, New
Jersey, Marekani na anamiliki jumba lenye thamani ya Dola 17 milioni (Sh 26
bilioni).
Pia ana magari kibao yakiwamo Chevloret, Royce
Royce Phantom, Ferrari na Range Rover.
Post a Comment